Sengerema, 12/03/2020:
Mamlaka ya
Hali ya Hewa Tanzania (TMA) iliandaa warsha na kukutana na wadau kutoka sekta ya uvuvi katika Ziwa
Victoria, kwa wilaya ya Muleba il tarehe 10 Machi, 2020 na Sengerema tarehe 12 Machi,
2020. Lengo la warsha ilikuwa ni kutoa Elimu Kuhusiana na usambazaji na
matumizi ya huduma na taarifa za Hali ya Hewa Zinazozingatia Athari (A workshop
on dissemination and the use of Impact Based Early Warning products)
Katika
ufunguzi wa warsha iliyofanyika wilayani Muleba mgeni rasmi alikuwa Mhe. Emmanuel
Shilembi ambaye aliipongeza TMA kwa kazi nzuri inayoifanya ya kuendelea kuboresha
utoaji wa huduma za hali ya hewa kwa wananchi hususan wavuvi wanaotumia Ziwa
Victoria kama kitega uchumi cha kuendesha maisha yao ya kila siku.
“Ninawapongeza
sana TMA kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuendelea kuboresha huduma za hali ya
hewa kwa wananchi hususan watumiaji wa Ziwa Viktoria, huduma hizo zimechangia
kwa Kiasi kikubwa kupunguza majanga yatokanayo na hali mbaya ya hewa”. Alisisitiza
Mhe. Emmanuel Shilembi
Aidha, mwakilishi
wa Mkurugenzi Mkuu wa TMA ndugu. Steven Malundo aliwashukuru wadau kwa kuitikia
wito wa kushiriki katika warsha hiyo muhimu pamoja na kuelezea kuwa warsha hiyo
ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) wa
kuboresha huduma za hali ya hewa kwa watumiaji wa Ziwa Viktoria uitwao “HIGH Impact
Weather IAke sYstems (HIGHWAY), ambao kwa hapa Tanzania unatekelezwa katika
wilaya za Sengerema-Mwanza na Muleba-Kagera kwa ufadhili wa Shirika la
Maendeleo la Uingereza (DFID).
No comments:
Post a Comment