Mhe. Mhandisi. Atashasta
Nditiye akihutubia
Baraza la Wafanyakazi, TMA, lililofanyika Dodoma Tarehe 16 na 17 Machi,
2020.
|
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TMA Bi. Jane
Kikunya, akitoa neno kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi wa Baraza la Wafanyakazi
TMA, lililofanyika Dodoma Tarehe 16
na 17 Machi, 2020.
|
Meneja Rasilimali Watu na msimamizi wa Divisheni ya Huduma Saidizi wa TMA, akitoa maelezo mafupi katika Baraza la Wafanyakazi TMA, lililofanyika Dodoma Tarehe 16 na 17 Machi, 2020. |
Mwenyekiti wa TUGHE - TMA, Bi. Aurelia Mwakalukwa akiwasilisha
taarifa ya TUGHE - Makao Makuu TMA katika Baraza la Wafanyakazi TMA, lililofanyika Dodoma Tarehe 16 na 17
Machi, 2020
|
Mwenyekiti wa TUGHE – Zanzibar Ndg. Awesi Kheri Awesi akiwasilisha Salamu za
TUGHE - Zanzibar katika Baraza la Wafanyakazi TMA, lililofanyika Dodoma Tarehe 16 na 17
Machi, 2020
|
Mwenyekiti kinamama Zanzibar Bi. Zaituni Khamis akiwasilisha Salamu za
kinamama Zanzibar katika Baraza la Wafanyakazi TMA, lililofanyika Dodoma Tarehe 16 na 17
Machi, 2020
|
Mwenyekiti kinamama TMA - Makao Makuu, Bi. Zainab Gumbo
akiwasilisha Salamu za kinamama wa TMA katika Baraza la Wafanyakazi TMA,
lililofanyika Dodoma Tarehe 16 na 17 Machi, 2020
|
Mfanyakazi bora wa TMA, Ndg. Kisumo Msangi kutoka kituo
cha TMA - Arusha akizungumza katika Baraza la Wafanyakazi TMA,
lililofanyika Dodoma Tarehe 16 na 17 Machi, 2020
|
Mwakilishi toka TUGHE akimtambulisha mfanyakazi bora wa
TMA 2020 katika Baraza la Wafanyakazi TMA, lililofanyika Dodoma Tarehe 16
na 17 Machi, 2020
|
Watoa mada wakiwasilisha mada za mkataba mpya wa baraza
na mkataba mpya wa hali bora kazini, Ukimwi na Korona katika Baraza la
Wafanyakazi TMA, lililofanyika Dodoma Tarehe 16 na 17 Machi, 2020
|
Waalikwa wa Baraza la Wafanyakazi la TMA wanaotarajia
kustaafu mwaka huu 2020 wakiaga wajumbe wa Baraza hilo katika Baraza la
Wafanyakazi TMA, lililofanyika Dodoma Tarehe 16 na 17 Machi, 2020
|
Meza Kuu, wakati wa ufunguzi rasmi wa Baraza la
Wafanyakazi TMA, lililofanyika Dodoma Tarehe 16 na 17 Machi, 2020
|
Meza Kuu, wakati wa uchaguzi wa mfanyakazi bora katika Baraza
la Wafanyakazi TMA, lililofanyika Dodoma Tarehe 16 na 17 Machi, 2020
|
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi TMA, wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika baraza hilo lililofanyika Dodoma Tarehe 16 na 17
Machi, 2020
|
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi TMA, wakiwakumbuka
wajumbe wa Baraza hilo waliofariki katika baraza hilo lililofanyika Dodoma Tarehe 16 na 17
Machi, 2020
|
Wajumbe wa Baraza la wafanyakazi la TMA katika picha ya
pamoja na mgeni Rasmi Mhe. Mhandisi.
Atashasta Nditiye katika baraza hilo
lililofanyika Dodoma Tarehe 16 na 17 Machi, 2020
|
Mjumbe wa Baraza, Meneja wa Kanda ya Nyanda za juu
Kusini Ndg. Issa Hamad akiwasilisha maazimio ya Baraza la wafanyakazi wa TMA katika baraza hilo lililofanyika
Dodoma Tarehe 16 na 17 Machi, 2020
|
Dodoma,
Tarehe: 16/03/2020;
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi
na Mawasiliano) Mhe. Mhandisi. Atashasta Nditiye ameagiza wajumbe wa Baraza la
wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuandaa miongozo na
mafanikio yenye tija kwa Mamlaka na Serikali
kupitia mijadala ya Baraza hilo.
Mhe. Mhandisi. Nditiye alitoa maagizo hayo wakati
akifungua Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) linalofanyika
katika Ukumbi wa Takwimu, Dodoma, Tarehe 16 na 17 Machi 2020.
“Hakikisheni
kwamba mnaweka vyema vipaumbele vyenu, na kutimiza mambo ya msingi kwanza ili
kukabiliana na tatizo la ufinyu wa bajeti lililopo”. Alisema Mhe. Mhandisi. Nditiye
Aidha Mhe. Naibu Waziri aliitaka Mamlaka
kuharakisha upatikanaji wa kanuni ili sheria ianze kufanya kazi kurahisisha
ufanisi wa majukumu ya Mamlaka.
“Endeleeni kuboresha utabiri na kutoa tahadhari za hali
mbaya ya hewa kwa wakati na kwa usahihi kwa jamii ya watanzania na wageni wanaotembelea
nchini, kwa kusema hivi naamini michango yenu katika mkutano huu wa Baraza lenu
la wafanyakazi, itatoa matokeo makubwa yatakayoendeleza sekta ya hali ya hewa
nchini na pia kuliwezesha Taifa letu kusonga mbele kiuchumi na kimaendeleo”. Alisisitiza Mhe. Mhandsi. Nditiye.
Naye,
Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa
Duniani (WMO) Dkt. Agnes Kijazi alimshukuru Mhe. Naibu Waziri kwa kujumuika na
wajumbe wa Baraza katika ufunguzi wa Baraza hilo na Wizara kwa ujumla kwa
ushirikiano mkubwa iliyoonesha katika kuboresha muundo mpya wa Mamlaka unaolenga
kuboresha maslahi ya wafanyakazi..
“Uwepo
wako umetupa nguvu na ari mpya katika kutekeleza majukumu yetu kwa ufanisi
zaidi hasa katika kipindi hiki ambacho TMA imekuwa Mamlaka kamili”.Alieleza
Dkt. Kijazi
Aliendelea
kwa kumueleza kuwa Baraza la mwaka huu ni kwa mujibu wa mkataba mpya kati ya Menejiment
na TUGHE na linajumuisha wajumbe 98 kutoka vituo mbali mbali vya hali ya hewa
hapa nchini ikijumuisha viongozi na wawakilishi wa wafanyakazi.
Kwa
upande wake mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Bi Jane Kikunya alimuomba
Mhe. Naibu Waziri kusaidia katika kutatua changamoto ya ufinyu wa bajeti kwa kuongeza
zaidi bajeti kwaajili ya kusaidia uboreshaji wa vifaa vya hali ya hewa
Mkutano
huo wa Baraza ulianza na elimu ya namna ya kukabiliana na maambukizi ya virusi
vya Korona katika maeneo yao ya kazi na jamii kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment