Washiriki
wa mafunzo ya Udhibiti na Ukusanyaji wa
Mapato yaliyoandaliwa mahususi kwa Menejiment ya TMA, Dodoma, Tarehe 13 Machi
2020 katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
|
Baadhi ya washiriki wa
mafunzo wakipokea vyeti vya ushiriki wa mafunzo
ya Udhibiti na Ukusanyaji wa Mapato
yaliyoandaliwa mahususi kwa Menejiment ya TMA, Dodoma, Tarehe 13 Machi 2020.
|
Dodoma,
Tarehe: 13/03/2020;
Msajili wa Hazina Ndugu. Athumani Selemani Mbuttuka
ameiagiza Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuchangia katika mfuko wa
serikali kupitia ukusanyaji wa mapato. Hayo yalizungumzwa wakati akifunga
Mafunzo ya Udhibiti na Ukusanyaji wa Mapato yaliyoandaliwa mahususi kwa
Menejiment ya TMA, Dodoma, Tarehe 13 Machi 2020.
“Kupitia Ofisi yangu tutaendelea kuwasaidia na
kuwapa ushirikiano katika kutimiza majukumu yenu mapya mliyokasimiwa kisheria.
Aidha, nawakumbusha jukumu kubwa la kuongeza mapato na kuchangia katika mfuko
wa serikali”. Alisema Bw. Mbuttuka
Aliendelea kusisitiza kuwa, ujuzi
uliopatikana utumike vizuri ili kusimamia vizuri zaidi jukumu jipya la udhibiti
ambalo ni la kisheria pamoja na kuboresha majukumu ambayo TMA ilikuwa nayo
kabla ya kuwa Mamlaka.
“Nipende kurudia tena kuwa, pale
mtakapohitaji ushauri kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina msisite kuja kwani
lengo letu ni pamoja na kujenga Tanzania ya viwanda na kukuza uchumi wetu ili
kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 ambapo TMA ina mchango mkubwa”.
Alisisitiza Msajili wa Hazina.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la
Hali ya Hewa Duniani (WMO) Dkt. Agnes Kijazi alisema kuwa mafunzo yameongeza
morali ya kuendelea kuboresha huduma za hali ya hewa hapa nchini ili kukidhi
mahitaji ya wadau kote nchini na pia yametoa uelewa wa kutosha katika eneo la
kudhibiti na kuongeza mapato.
“Napenda
nikuahidi mheshimiwa mgeni rasmi kwamba tutayaweka mafunzo haya katika matendo
na kuisimamia vyema sheria iliyoanzisha TMA ili kuhakikisha wote wanaotumia
huduma za hali ya hewa kibiashara wanachangia huduma hizo”.Alieleza Dkt. Kijazi
Aliendelea
kufafanua mafunzo yaliyofanyika yameongeza uelewa kwa Menejiment ya Mamlaka ya
Hali ya Hewa kuhusu jukumu jipya walilopatiwa la kudhibiti huduma za hali ya
hewa hapa nchini.
Naye,
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya
Mtandao (TaGLA), Ndugu, Charles Senkondo alifurahishwa na jinsi washiriki
hao ambao ni viongozi kutoka TMA walivyoonesha kunufaika na mafunzo hayo ambapo
ndiyo dhumuni la TaGLA kusikia hivyo na si vinginevyo.
Awali,
Mwezeshaji kutoka Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) Ndugu, Felix
Ngamlagosi alieleza namna washiriki hao walivyoonesha dhamira (commitment) na
ushirikiano wa hali ya juu katika kuhakikisha wanafikia lengo la mafunzo hayo
Mafunzo
hayo ya siku tano yaliandaliwa na TMA kwa kushirikiana na TaGLA, yamejumuisha viongozi
kutoka katika ofisi za TMA zilizoko kwenye kanda nane za Mamlaka ikiwa pamoja
na Ofisi ya Zanzibar.
No comments:
Post a Comment