Chama cha
Wataalamu wa Hali ya Hewa Tanzania (Tanzania Meteorological Society-TMS)
kimewapongeza Dkt. Buruhani Nyenzi ambaye pia ni rais wa chama hicho kwa
kuchaguliwa kuwa makamu rais wa Jukwaa la Kimataifa la Wataalamu wa hali ya hewa
( International Forum of Meteorological Societies- IFMS) na Dk. Agnes Kijazi,
Mkurugenzi Mkuu wa TMA kwa kuteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) kuwa
mjumbe wa Jopo la wataalam kumi (10-member Group) lenye jukumu la kumshauri
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu namna ambavyo sayansi, teknolojia na
ubunifu (STI) zinavyoweza kutumika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu ya
umoja huo (Sustainable Development Goals(SDGs).
Pongezi hizo
zilitolewa katika mkutano wa TMS uliofanyika jijini Dar es Salaam kwa kujumuisha
wanachama wa TMS kutoka maeneo mbali mbali nchini. Makamu wa rais wa TMS Dkt.
Clavery Tungaraza kutoka chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) na Katibu wa TMS
Dkt.Ladislaus Chang'a kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) kwa pamoja walisema
mafanikio hayo ni mafanikio ya TMS kwani Dkt. Nyenzi na Dkt.Kijazi ni wanachama
wa TMS.
Tunampongeza
sana rais wa Umoja wetu Dkt. Nyenzi kwa kuchaguliwa kuwa makamu wa rais wa IFMS
na Dkt. Kijazi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa kwa kuteuliwa na Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwa miongoni mwa wajumbe wa Jopo la wataalam kumi (10)
kuunda kamati ya Umoja wa Mataifa (UN) ya kumshauri Katibu Mkuu wa Umoja huo, tunatambua
nafasi hizi ni fahari kwa wana TMS wote kwani ni fursa kwa TMS kuitangaza nchi yetu kimataifa ‘alisema Dkt.
Tungaraza’
Kwa upande
wake Dkt. Nyenzi aliwashukuru sana wanachama wote kwa pongezi na kusisitiza
ushirikiano ili aweze kuipeperusha vyema bendera ya nchi kimataifa. Jukwaa lile
ni la kimataifa hivyo mtanzania kuwa miongoni mwa viongozi wa juu wa jukwaa (forum)
hilo ni jambo la kujivunia sisi kama wana TMS na nchi yetu kwa ujumla. Akipokea
pongezi hizo Dkt. Kijazi aliwashukuru wanachama na kufafanua kwamba wao kama
wana sayansi mawazo yao ni muhimu katika kumuwezesha kutekeleza jukumu hilo
kubwa la kimataifa. Uteuzi huu ni fahari kwa TMS na nchi yetu kwa ujumla hasa
ikizingatiwa kwamba katika kundi la watu kumi tu kwa dunia nzima Tanzania nayo
inatajwa ‘alisema Dkt. Kijazi.’
Wakati huo
huo wanachuo waliomaliza na kufanya vizuri kwa masomo ya elimu ya shahada ya
sayansi ya hali ya hewa (Bsc. Meteorology) kwa mwaka 2017 Bi. Aisha Nassor
(mwanafunzi bora wa jumla), Bi. Leila Muhoma na Bw. Kekazuri Elly walipongezwa
kwa jitihada zao na kupatiwa zawadi ya cheti na fedha taslim. Akikabidhi zawadi
hizo Dkt. Kijazi alisema anafurahishwa kuona wanawake wanaongoza katika mafunzo
hayo ya BSc Meteorology yanayotolewa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Kwa upande wake Dkt. Nyenzi aliwajulisha wanachama kwamba TMS itaendelea
kuwapongeza wanafunzi wanaofanya vizuri kwa lengo la kuchangia katika
kuendeleza taaluma ya hali ya hewa hapa nchini.
Imeandaliwa
na;
Ofisi ya
Uhusiano
Mamlaka ya
Hali ya Hewa Tanzania(TMA)
|
No comments:
Post a Comment