15/11/2018, Kigoma.
Kaimu Katibu Mtendaji wa
NACTE Mhandisi, Dkt. Annastellah Sigwejo amekipongza Chuo cha Taifa cha Hali ya
Hewa ‘NMTC’ kwa jitihada zake za kukitangaza chuo kitaifa na kimataifa. Pongezi
hizo zilitolewa wakati wa uzinduzi wa tovuti na nembo mpya ya chuo hicho.
‘Nawapongeza kwa kuhakikisha kunakuwa na tovuti ya chuo ikiwa ni moja ya
vitu ambavyo NACTE inahimiza, aidha tovuti ya chuo ni muhimu sana na ina faida kubwa kwani hukitangaza chuo kwa upana sana
kitaifa na kimataifa’. Alisema Dkt. Sigwejo.
Vile vile, aliongezea kwa
kusema, ‘kwa vile tovuti hii imeunganishwa na tovuti-mama ambayo ni ya Mamlaka
ha Hali ya Hewa Tanzania ‘TMA’ itasaidia pia watumiaji kupata taarifa za hali
ya hewa nchini ambazo ni za muhimu sana kwa wananchi kwa sekta zote za
maendeleo ya nchi pamoja na wananchi kwa ujumla wake’.
Aliendelea kwa kuelezea
kuwa kwa taarifa aliyonayo ni kwamba kuna vyuo viwili tu vya hali ya hewa katika
ukanda wa Afrika Mashariki, hivyo kwa kupitia tovuti ya chuo, chuo kitajulikana
zaidi au kitawafikia watu wengi zaidi ndani ya nchi na nje ya nchi na hivyo
kuongezeka kwa udahili, muhimu ni kuhakiksha vigezo vya utoaji elimu vinafuatwa.
Uzinduzi wa tovuti (www.nmtc.ac.tz)
na nembo ya chuo ulifanyika rasmi tarehe 15 Novemba 2018, katika ukumbi wa chuo
cha NMTC-Kigoma na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu manispaa
ya Kigoma.
Chuo cha Taifa
cha Hali ya Hewa (National Meteorological Training Centre (NMTC) ni chuo
kilicho chini ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na ni chuo pekee nchini
kinachotoa taaluma ya hali ya hewa katika ngazi ya cheti (NTA-Level 5) na
diploma (NTA-level 6). Chuo kimesajiliwa kwa usajili wa kuduma mwaka 2014 na Baraza
la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ili kutoa elimu bora yenye kukidhi
viwangona kwa sasa kipo katika mchakato wa kupata ithibati (Accreditation).
IMETOLEWA NA OFISI YA
UHUSIANO
MAMLAKA YA HALI YA HEWA
TANZANIA
No comments:
Post a Comment