Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania (TMA) pamoja na wadau
mbalimbali wa sekta ya utalii wamejumuika katika kuadhimisha mwezi wa Urithi
Festival kwa mkoa wa Dar es Salaam yanayofanyika Kijiji cha Makumbusho,
Kijitonyama Tarehe 01 hadi 06 Oktoba 2018.
Katika maonesho hayo
TMA ambayo ni taasisi iliyopewa jukumu la kutoa huduma za hali ya hewa
nchini imeendelea kutoa elimu namna ya kuulinda na kuutunza urithi wa nchi yetu
kwa kutambua faida za matumizi ya taarifa za hali ya hewa.
Miongoni mwa elimu inayotolewa ni matumizi ya taarifa
za hali ya hewa za muda mfupi, kati,
mrefu na takwimu za hali ya hewa katika
kulinda mali kale mfano majengo ya zamani yaliyo kando ya fukwe za bahari
ambapo kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa/tabia nchi utafiti unaonesha
uwepo wa ongezeko la kina cha bahari hivyo kupelekea uwezekano wa kupotea kwa
urithi wa nchi hii. Aidha kuhamahama kwa wanyama kutokana na kutafuta malisho,
ikumbukwe kuwa uoto wa asili hutegemea hali ya hewa nzuri kama vile mvua za
kutosha
Vilevile, kwa upande wa kilimo watanzania wana
shauriwa kuhakikisha taarifa za hali ya hewa zinafuatwa ili kuweza kuendelea
kulima na kuzalisha mazao ya asili kwa jamii. Pamoja na hayo TMA pia hutoa
taarifa za hali ya hewa zinazosaidia kuchagua vazi la asili la kuvaa kwa
kipindi husika kama vile baridi, joto n.k
Ngoma na michezo ya asili pia hutegemea hali ya hewa
ya eneo husika kama vile upepo mkali, mvua kubwa kwa maeneo ya michezo ya
ziwani, viwanjani n.k
TMA inawakaribisha wananchi wote kufika katika banda
lake ili kuweza kujifunza mengi yanayohusu hali ya hewa na maliasili na utalii
(urithi wetu)
IMETOLEWA NA KITENGO CHA UHUSIANO
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
No comments:
Post a Comment