Baadhi
ya waandishi walioshiriki mkutano wa wanahabari wa kutoa mwelekeo wa mvua za Msimu
kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua
Mamlaka
ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa rasmi utabiri wa msimu kuanzia mwezi
Novemba, 2018 hadi Aprili, 2019 katika mkutano wa waandishi wa habari
uliofanyika katika Ofisi za TMA. Mkutano huo uliudhuriwa na wajumbe wa Bodi ya
Ushauri wa TMA wakiongozwa na mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Buruhani Nyenzi
Taarifa
hiyo inatoa uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa mvua
za Msimu kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua (kanda ya magharibi,
kati, nyanda za juu kusini magharibi, kusini mwa nchi, ukanda wa pwani ya
kusini pamoja na maeneo yaliyoko kusini mwa mkoa wa Morogoro) katika kipindi
cha miezi ya Novemba, 2018 hadi Aprili, 2019. Aidha, taarifa imeendelea kwa kutoa
mrejeo wa mvua za Vuli katika maeneo ya ukanda wa ziwa Victoria, pwani ya
kaskazini na nyanda za juu kaskazini-mashariki.
Vile
vile, ushauri na tahadhari umetolewa kwa wadau wa sekta mbali mbali wanaotumia
taarifa za hali ya hewa katika utekelezaji wa majukumu yao kama vile kilimo na
usalama wa chakula, mifugo na wanyamapori, maliasili na utalii, uchukuzi na
mawasiliano, nishati na maji, mamlaka za miji, afya pamoja na menejimenti za maafa.
Kusoma zaidi ingia humu http://www.meteo.go.tz/pages/climate-outlook-for-msimu-rains-nov-2018-apr-2019
No comments:
Post a Comment