Mtaalamu wa hali ya hewa kutoka TMA akiwasilisha mada
|
Pichani ni wadau kutoka katika sekta mbalimbali wakitoa maelezo ya mchango wa taarifa za hali ya hewa katika utekelezaji wa majukumu yao. |
|
Pichani
ni Makundi mbalimbali yakijadili namna wanavyoweza kuutumia Utabiri wa
Hali ya Hewa katika utekelezaji wa majukumu katika sekta mbalimbali hapa
nchini na baadae kuwasilisha kwa wajumbe |
|
Katikati ni kaimu mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa dkt. Ladislaus Chang'a kwenye picha ya pamoja na washiriki kwenye warsha ya wadau kutoka sekta mbalimbali walipokutana na wataalamu wa hali ya hewa kujadili mvua za msimu wa Novemba 2018 hadi Aprili 2019 | | |
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) leo tarehe
11/10/2018 imekutana na wadau kutoka sekta ya maafa, afya, kilimo,
nishati, mazingira,mipango miji na wanahabari kujadili matarajio na
mwelekeo wa mvua za msimu kwa maeneo yanayopata mvua mara moja kwa mwaka
kuanzia mwezi Novemba 2018 hadi Aprili 2019 ili kuongeza uelewa wa
taarifa za hali ya hewa kwa sekta mbalimbali zinazoathirika zaidi na
hali ya hewa.
Aidha,
wadau walipata nafasi ya kujadili mwenendo wa utabiri wa msimu wa vuli
(Oktoba hadi Desemba 2018) uliotolewa 05 Septemba 2018 ambao unaonesha
kuwa mvua zimeanza (onset) kama ilivyotabiriwa kwa maeneo mengi ingawaje
mtawanyiko wake bado haujaimarika hali inayosababishwa na mgandamizo
mdogo wa hewa uliopo Mashariki mwa Pwani ya Somalia unaoathiri mifumo ya
hali ya hewa
Kwa upande
wa mdau kutoka wizara ya afya bw.Stephen Kiberiti aliwashukuru TMA kwa
utaratibu wa kukutana na wadau hii inasaidia sekta husika kujiandaa na
athari zinazoweza kujitokeza.
Mikoa inayopata mvua mara moja kwa mwaka ni Dodoma, Singida, Katavi, Mbeya,Tabora, Kigoma(ukitoa Kigoma Kaskazini), Mtwara, Lindi,Ruvuma, Iringa, Songwe, Rukwa, Njombe na Kusini mwa Morogoro
Warsha
hii imedhaminiwa na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) kupitia mradi
wa mfumo wa kidunia wa huduma za hali ya hewa Duniani (Global Framework
for Climate Service-GFCS)
|
No comments:
Post a Comment