Friday, August 31, 2018

MAADHIMISHO YA WIKI YA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI:TMA YASHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA KUTOA ELIMU YA UHUSIANIO KATI YA SHUGHULI ZA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

Meneja wa TMA kanda ya kati Bw. Waziri Waziri akifafanua jambo kwa mwananchi aliyetembelea banda la TMA kwenye maadhimisho ya Jeshi la zimamoto na uokoaji yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri, Dodoma



Mtaalamu wa hali ya hewa kutoka TMA kanda ya kati Bw. Zeno Chaula  akifafanua jambo kwa mwananchi aliyetembelea banda la TMA kwenye maadhimisho ya Jeshi la zimamoto na uokoaji yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri, Dodoma



Wanafunzi wakipata Elimu ya umuhimu wa tarifa za hali ya hewa kwa sekta mbalimbali walipotembelea banda la TMA kwenye maadhimisho ya Jeshi la zimamoto na uokoaji yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri, Dodoma



Matukio mbalimbali katika picha kwenye maadhimisho ya Jeshi la zimamoto na uokoaji yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri, Dodoma

Thursday, August 30, 2018

LUGOLA: USAHIHI WA UTABIRI WA HALI YA HEWA NI WA KIWANGO CHA JUU

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola akipata maelezo kutoka kwa meneja wa TMA kanda ya kati   Bw. Waziri Waziri katika banda la TMA kwenye maadhimisho ya wiki ya zimamoto na uokoaji, mkoani Dodoma.


DODOMA.



Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imejumuika na taasisi zingine kuadhimisha wiki ya jeshi la zimamoto na uokoaji kitaifa inayofanyika Jijini Dodoma tarehe 29 Agosti hadi 01 Septemba 2018. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Shiriki kukuza uchumi wa viwanda, funga king’amua moto kwenye kiwanda chako.” 



Maadhimisho hayo yalifunguliwa rasmi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola (MB) ambaye alitembelea banda la TMA na kuwapongeza kwa usahihi wa hali ya juu wa utabiri wa hali ya hewa unaotolewa kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni na kuwataka waendelee kuboresha ili kufikia viwango vya  juu zaidi ya  walipo kwa sasa. Mhe. Lugola aliweza kupata maelezo mafupi kutoka kwa meneja wa TMA kanda ya kati  Bw. Waziri Omari Waziri ambapo alieleza kuwa taarifa za hali ya hewa ni muhimu kwa shughuli za uokoaji na zimamoto, akitolea mfano taarifa za upepo mkali ambao kwa kiasi kikubwa unaweza kusababisha moto kusambaa kwa  kasi (eneo kubwa) au hata kwa watumiaji wa bahari au ziwa kuathirika na mawimbi makubwa vile vile taarifa ya mvua kubwa inayotarajiwa kunyesha katika eneo husika zinasaidia vikosi vya uokoaji kujipanga na vifaa na njia ya uokoaji kutokana na hali ya hewa ya eneo husika. Aliongezea kuwa mchango wa taaarifa za hali ya hewa katika kukuza uchumi wa maendeleo ya viwanda ni pamoja na kutambua hali ya hewa ya eneo husika ili kujua namna ya kuwekeza, mfano mwelekeo wa upepo hii inasaidia kujua jinsi ya kuelekezea uchafu (moshi), kiasi cha uzalishaji kama vile vinywaji baridi kwa kipindi cha baridi au joto, usafirishaji wa mazao ya viwandani hutegemea hali ya hewa ya wakati huo sambamba na miundo mbinu mfano kipindi cha mvua kubwa ambacho husababisha uharibifu wa miundo mbinu hivyo ni vyema mwekezaji akatafuta njia mbadala ya usafirishaji na mengine mengi.



IMETOLEWA NA KITENGO CHA UHUSIANO, MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Tuesday, August 28, 2018

WANASAYANSI WA HALI YA HEWA NCHINI (METEOROLOGISTS) WAKUTANA KUANDAA MWELEKEO WA HALI YA HEWA KWA KIPINDI CHA MWEZI OKTOBA HADI DESEMBA 2018

WANASAYANSI WA HALI YA HEWA NCHINI (METEOROLOGISTS) WAKUTANA KUANDAA MWELEKEO WA HALI YA HEWA KWA KIPINDI CHA MWEZI OKTOBA HADI DESEMBA 2018

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA)  ikiwa katika maandalizi ya kutoa utabiri/mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli imeandaa mkutano wa wanasayansi wa hali ya hewa (meteorologists) kujadili rasimu ya mwelekeo huo.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo, mgeni rasmi ambaye ni mkurugenzi mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi amewataka wataalam hao kuandaa kwa pamoja na kupitia mfumo mzima wa uaandaaji ili kujiridhisha  na utabiri utakao tolewa hapo baadae sambamba na kutoa mapendekezo ya uboreshaji katika maandalizi mengine ya misimu ijayo. Aidha Dk. Kijazi aliwapongeza wanasayansi hao kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kutoa utabiri wenye viwango vya juu vya usahihi kwa zaidi ya asilimia 80 na kuwataka waendelea kufanya kazi kwa bidii na ushirikiano ili kufikia juu ya asilimia 90.

Hii ni mara ya kwanza kwa TMA kuwakutanisha wanasayansi kutoka vituo vyote nchini ambapo awali kazi ya uandaaji utabiri ilikuwa ikifanywa na wanasayansi wa makao makuu na uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (JNIA) pekee

TMA inatarajia kutoa mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli kwa mikoa inayopata mvua mara mbili kwa mwaka tarehe 06 Septemba 2018.

IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

KATIBU MKUU SHIRIKA LA HALI YA HEWA DUNIANI(WMO) ASIFU JITIHADA ZA SERIKALI KATIKA KUBORESHA HUDUMA ZA HALI YA HEWA NCHINI.


Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye tarehe 21 Agosti 2018 amekutana  na Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas katika ofisi za Wizara ya Uchukuzi ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi ambapo atashiriki katika uzinduzi wa mfumo wa taifa wa huduma za hali ya hewa na kutembelea ofisi za TMA tarehe 22 Agosti 2018.

Akizungumza na vyombo vya habari, Mhe. Nditiye amesema ni heshima kubwa kwa Tanzania kupata ugeni huu kwa vile WMO wamekuwa wakitoa miongozo mbalimbali katika utekelezaji wa huduma za hali ya hewa kwenye nchi wanachama ikiwemo Tanzania. Aidha wamekuwa wakiwajengea uwezo TMA kupitia mafunzo ya wataalam na upatikanaji wa baadhi ya vifaa vya hali ya hewa.

Kwa upande wa Katibu Mkuu huyo wa WMO alisema, amekuwa akishuhudia mazuri mengi kuhusiana na Tanzania hususani kupitia TMA ambayo ni moja ya taasis bora za hali ya hewa barani Afrika. Aidha alifafanua kwamba mafanikio hayo yametokana  na juhudi za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuboresha miundombinu ya hali ya hewa ikiwemo kupatikana kwa rada za hali ya hewa.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi alisema katibu mkuu huyo atakuwepo nchini kujionea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na TMA katika kutekeleza makubaliano ya kimataifa yaliyofikiwa kupitia Shirika la Hali ya Hewa Duniani.

Katika mkutano huo alikuwepo pia Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Leonard Chamuriho ambapo alifurahishwa  na maelezo aliyoyatoa katibu mkuu huyo kwamba WMO itaendelea kushirikisha taasis za hali ya hewa za Afrika ikiwemo TMA. 


Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...