Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dkt. Agnes Kijazi katika picha ya
pamoja na washiriki wa warsha hiyo.
Mamlaka ya Hali ya
Hewa Tanzania (TMA) kwa kushirikiana na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO)
wameandaa mafunzo ya hali ya hewa kwa
kutumia modeli ya PRECIS (Providing
Regional Climates for Impact Studies) kuanzia tarehe 29 Juni hadi 03 Julai 2015. Warsha/ mafunzo haya yameandaliwa na
TMA chini ya mwamvuli wa mradi wa GFCS unaotekelezwa kwa upande wa Afrika
katika nchi za Tanzania na Malawi
Washiriki wa mafunzo
hayo kutoka TMA na Kurugenzi ya Hali ya Hewa ya Malawi wanategemea kujifunza matumizi ya modeli ya
PRECIS kutoka kwa mtaalamu kutoka Ofisi ya Hali ya Hewa ya Uingereza ambayo
imekuwa ikitumia modeli hiyo katika utekelezaji wa huduma za hali ya hewa.
Lengo kuu la mafunzo
hayo ni kuongeza uelewa wa utoaji huduma za hali ya hewa pamoja na kuweza kutoa
taarifa sahihi za muda mrefu zenye kuweza kukabiliana na changamoto za
mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi. Alisema
Dkt.Kijazi
PRECIS ni mfumo unaweza kutoa taarifa za hali
ya hewa za muda mrefu (Klimatolojia) kwa eneo husika.
Imetolewa na Monica Mutoni, Afisa Uhisiano.
TMA
No comments:
Post a Comment