Wanasayansi ya hali ya hewa (Meteorologists) wamekutana katika warsha ya siku moja iliyofanyika tarehe 06 Julai 2015 katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA). Warsha hiyo ambayo ulikuwa na lengo la kujadili masuala mbalimbali yakiwemo kubobea (specialization) katika matumizi ya sayansi ya hali ya hewa kwenye sekta mbalimbali kama vile kilimo, afya, nishati, maji, usafiri wa anga na kwenye maji n.k; ushiriki wa TMA katika kuchangia masuala ya hali ya hewa ya kikanda na kimataifa, na wataalam kujikita katika tafiti zenye kuchangia katika maendeleo ya taifa letu.
Akizungumza katika warsha hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TMA
Dkt. Agnes Kijazi alisema dhumuni ni
kuangalia changamoto zinazokabili sayansi ya hali ya hewa hasa katika kipindi
hiki cha mabadiliko ya tabia nchi hivyo basi kuangalia jinsi ya kuboresha
taaluma ya hali ya hewa ikiwa ni pamoja na
kufanya tafiti zenye tija kwa maedeleo ya nchini yetu. Aidha alielezea pia
umuhimu wa kubobea (specialization) kwenye utoaji wa huduma za hali ya hewa kwa
sekta zingine.
Dkt Kijazi aliongeza kwa kusema, warsha kama
hizi ni fursa nzuri kwa wanasayansi
kutambua nafasi zao na mchango wao wa kutoa
huduma bora za hali ya hewa kwa jamii.
Warsha hiyo imeandaliwa katika mpango wa TMA
kuboresha huduma zake ili kufikia dira waliyojiwekea ya kuwa kitovu cha ubora
cha utoaji huduma za hali ya hewa ‘Centre of excellence in provision of
meteorological services’
Dkt. Agnes Kijazi akisisitiza jambo kwa wanasayansi katika warsha ya siku moja ya wataalamu hao.
Baadhi ya wanasayansi ya hali ya hewa kutoka Makao Makuu ya TMA na ofisi za JNIA wakimsikiliza kwa makini maelezo ya Mkurugenzi Mkuu.
Imetolewa na :Monica Mutoni,
Ofisi ya Uhusiano- Mamlaka ya Hali ya Hewa
No comments:
Post a Comment