Monday, July 6, 2015

DK. KIJAZI ASISITIZA MATUMIZI YA MIFUMO YA MODELI ZA KISAYANSI.



Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dkt. Agnes Kijazi katika picha ya pamoja na wakufunzi wa mafunzo hiyo.



Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Dk.Agnes Kijazi amesisitiza matumizi ya mifumo ya modeli za Kisayansi. Akizungumza wakati akifunga mafunzo ya hali ya hewa kwa kutumia modeli ya PRECIS (Providing Regional Climates for Impact Studies) yalifanyika kuanzia tarehe 29 Juni hadi 03 Julai 2015., Dkt. Kijazi aliwataka wanawarsha kutumia utaalamu waliopata katika kuhakikisha wanaboresha utoaji huduma za hali ya hewa kwa maendeleo ya nchi. Aidha alitoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Norway, WMO na Ofisi ya Hali ya Hewa Uingereza kwa kuwezesha mafunzo hayo kupitia mpango wa GFCS.

Kwa niaba ya wanawarsha wote, Bw. Clement kutoka Malawi aliwashukuru wawezeshaji wote hususani TMA kwa kufanikisha mafunzo hayo na kuahidi kutumia utaalamu waliopata katika kuboresha taarifa za hali ya hewa kwa watumiaji maalum kama Kilimo na afya kwa maeneo husika.

Mafunzo hayo yalihusisha vipengele vilivyojikita katika ‘Modelling of the Earth Climate System’, ‘downscaling techniques, designing RCM experiments’, ‘LINUX’, ‘uncertainties in the model and data analysis’. Vipengele hivi vilikuwa muhimu sana kwa vile vitasadia katika kutatua changamoto za utoaji huduma za hali ya hewa kwa maendeleo ya taifa.


No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...