Dr. Kijazi amechaguliwa tarehe 4 June 2015 bila kupingwa wakati Mkutano Mkuu wa kumi na saba wa Shirika la hali ya Hewa Duniani(WMO-Congress wa 17) ulioanza tarehe 25 Mei ambao unatarajiwa kumalizika tarehe 12 June,2015 jijini Geneva, Uswis
Dr. Kijazi amechaguliwa
tarehe 4 June 2015 bila kupingwa wakati wa
Mkutano
Mkuu wa kumi na saba wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO
Congress wa 17) ulioanza tarehe 25 Mei ambao
unatarajiwa kumalizika tarehe 12 Juni, 2015
jijini Geneva, Uswisi
Kuchaguliwa kwa Dr. Agnes
Kijazi kumetokana na jitihada kubwa za Wizara
ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa kupitia Idara ya Ushirikiano wa
Kimataifa
na Ubalozi wetu wa Kudumu Umoja wa Mataifa, Geneva,
Dr. Kijazi
anaongoza ujumbe wa Tanzania katika ushiriki Mkutano huo ambao
una
washiriki kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Maji na Ubalozi wa
Tanzania, Geneva.
WMO ni Shirika la Umoja
wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya hali ya
hewa duniani na
mabadiliko ya tabia nchi. WMO inatekeleza majukumu na
maamuzi kuhusu
maendeleo ya sayansi ya hali ya hewa na uboreshaji wake
ikiwa ni
pamoja na kusimamia viwango katika upimaji na utoaji wa huduma za
hali ya hewa kwa nchi wanachama.
Hadi wakati wa Mkutano
huu unaoendelea nchini Uswisi, WMO ilikuwa na
nchi wanachama
191. Katika Mkutano huu nchi za Sudani ya Kusini na
Tuvalu zilikaribishwa rasmi kama wanachama wapya wa WMO. Kati ya
nchi
hizi 191 Wanachama wa WMO ni nchi 37 tu ambazo zina wajumbe
katika
Baraza hilo kuu. Hivyo hii ni nafasi adhimu na heshima kwa
Tanzania, TMA
na Dr Kijazi ambaye ni msomi mwenye
utaalamu wa kutosha akiwa na
shahada ya Uzamivu (Ph.D)
katika sayansi ya Hali ya hewa.
Kazi kuu ya Baraza la
Utendaji la WMO, ambalo Tanzania imefanikiwa kuwa
mjumbe ni kuchukua
hatua zinazostahili, kwa kushirikiana na Katibu Mkuu wa
Shirika
hilo kutekeleza maamuzi yanayotolewa na Mkutano Mkuu
(WMO-Congress) ambao hukutana mara moja kila baada ya miaka minne.
Akizungumza baada ya
uchaguzi huo Balozi Celestine Mushy, Mkurugenzi wa
Idara ya
Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa
Kimataifa alielezea sababu ya Tanzania kugombea nafasi hiyo muhimu ni
kutaka kuwa ndani ya chombo cha maamuzi na hivyo kushawishi maamuzi
yatakayoinufaisha jamii nzima ya kimataifa ikiwemo Tanzania katika
masuala
ya hali ya hewa ikiwa ni pamoja na kutoa
mwelekeo wa kisayansi katika
kukabiliana na athari za
mabadiliko ya hali ya hewa yanayoendelea maeneo
mengi Duniani.
Aidha, Dkt. Kijazi alieleza kuridhishwa kwake na jinsi ambavyo
nchi
wanachama 190 walivyoridhishwa na utendaji wa Tanzania katika kipindi
cha miaka mitatu (2012-2015) ambacho alikuwa mjumbe wa Baraza
hili na
hivyo kumchagua tena
katika kipindi kingine cha miaka minne.
“Hii ni heshima
kubwa kwa
nchi yangu ya Tanzania na ninaahidi kutumia uwezo wangu wote
kutekeleza majukumu ya nafasi hii” alisema Dkt. Kijazi.
Imetolewa na Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
No comments:
Post a Comment