Ujumbe
wa Tanzania unaendelea kushiriki katika kikao cha Mkutano Mkuu wa Kumi na saba
wa Shirikia la Hali ya Hewa Duniani (WMO-Congress 17), mijini Geneva, nchini
Uswisi. Ujumbe huo umeshiriki katika matukio mbalimbali ya mkutano huo ikiwa ni
pamoja na Dkt. Agnes Kijazi kushiriki katika siku ya Jinsia ya WMO (WMO Gender
Day), kutoa mada zilizotoa uzoefu wa Tanzania wa utekelezaji wa program za
utekelezaji wa programu ya utoaji wa huduma bora za hali ya hewa kwa jamii
“Global Framework for Climate Services (GFCS) na programu ya uendelezaji wa
mitandao ya upimaji wa hali ya hewa na mawasiliano (WMO Integrated Observation
System and WMO Information System-WIGOS/WIS). Kwa habari zaidi angalia picha za
matukio mbalimbali ya Mkutano huo hapa.
Mh.
Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Geneva na
Murugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Dkt. Agnes Kijazi na Ujumbe wa
Tanzania wakishiriki katika Mkutano Mkuu wa Kumi na Saba wa Shirika la Hali ya
Hewa Duniani (WMO- Congress-17), Geneva, Uswisi
“WMO Gender Day”, Siku ya Ijumaa, Tarehe 5 Juni
2015 ilikuwa siku ya Jinsia (WMO Gender Day) ya Mkutano wa Kumi na saba wa
Shirika la hali ya hewa Duniani (WMO-Congress 17). Dkt. Agnes Kijazi,
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania
katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) alikuwa miongoni mwa zaidi ya
wajumbe 50 na wafanyakazi wa WMO walioshiriki katika ufunguzi wa siku hii na
kujadili masuala mbalimbali katika nyanja ya usawa na uwezeshaji wa wanawake
katika taasisi za hali ya hewa na WMO. Maoni yaliyotokana na majadiliano ya
siku hii yatajumuishwa na kutengeneza Mpango Mkakati wa WMO utakaolenga masuala
ya jinsia (WMO Gender Action Plan)
Vile vile siku ya tarehe 6 Juni
2015, Dr. Kijazi alishiriki katika warsha ya Uongozi ya viongozi wanawake ikiwa
na lengo kuwajengea uwezo zaidi wa uongozi wajumbe waliohudhuria katika mkutano
mkuu wa kumi na saba wa WMO.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Dr Agnes Kijazi
akiwasilisha mada ya uzoefu wa Tanzania katika utoaji wa huduma za hali ya hewa
kwa jamii (Global Framework for Climate Services (GFCS)) katika Mkutano Mkuu wa
Kumi na Saba wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO Congress-17), Geneva,
Uswisi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dr. Agnes
Kijazi akiwasilisha mada ya uzoefu wa Tanzania katika utekelezaji wa Programu
ya "WMO Intergrated Global Observation Systems (WIGOS)" katika
Mkutano Mkuu wa kumi na saba wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Geneva,
Uswisi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dr. Agnes
Kijazi na Mkurugenzi wa utabiri Dr. Hamza Kabelwa wakiwa katika majadiliano na
maafisa wa Shirika la Hali ya hewa Duniani (WMO) na Marekani wakati wa
majadiliano yanayohusu namna ya kuboresha huduma za hali ya hewa kwa jamii
hususan utoaji wa tahadhari “ Early Warning” katika Mkutano Mkuu wa kumi na
saba wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Geneva, Uswisi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali
ya Hewa Tanzania (TMA), Dr. Agnes Kijazi na Mtabiri Mwandamizi katika Ofisi ya
Mahusiano ya Kimataifa ya TMA, Ndugu. Wilbert Timiza wakifuatili mwenendo wa
Mkutano Mkuu wa kumi na saba wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Geneva,
nchini Uswisi.
No comments:
Post a Comment