Bwana Wilberforce Kahwa Kikwasi (Mtabiri mwandamizi na
msimizi mkuu wa shughuli za uchambuzi na uandaaji wa utabiri wa hali ya hewa-Senior
Meteorologist and Head-Analyst Incharge) kituo kikuu cha utabiri wa hali ya
hewa Tanzania, mnamo tarehe 23 Juni 2015, katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu, alitununikiwa
nishani ya “Utumishi Mrefu, Maadili Mema na
ubunifu Daraja la Pili” na Mtukufu rais wa Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete”.
Nishani hii ni heshima kubwa kutoka kwa mtukufu rais
kwa kutambua mchango wa Bwana Wilberforce Kahwa Kikwasi na Mamlaka ya Hali ya
Hewa kwa ujumla katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Taifa kwa
kufanyakazi kwa uvumilivu, juhudi na weledi katika kutatua matatizo mbalimbali.
Bwana Wilberforce Kahwa Kikwasi amekuwa mbunifu kwa
kubuni mfumo kielektroniki wa ukusanyaji na mawasiliano ya taarifa na takwimu
za hali ya hewa (Digital Meteorological Observatory) ambao unaboresha huduma za
hali ya hewa na kupunguza gharama za uendeshaji.
Bodi ya ushauri ya Mamlaka ya Hali ya Hewa (MAB),
Menejimenti na wafanyakazi wote tunampongeza Bwana Wilberforce Kahwa Kikwasi
kwa heshima hiyo kubwa aliyoipata ambayo ni heshima kwetu sote.
Hivyo basi nishani hii iwe chachu kwa watumishi wote
wa TMA katika kujituma, kushirikiana, uvumilivu na kuwa na ubunifu. Kubwa zaidi
tudumishe mshikamano wetu ambao ndio siri kubwa ya mafanikio yetu.
“Hali ya Hewa kwa maendeleo endelevu”
IMETOLEWA
NA:
MONICA MUTONI
AFISA MAHUSIANO,
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
No comments:
Post a Comment