Dkt.
Agnes Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa na Mjumbe wa Kamati
Kuu ya Utendaji ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) katika picha ya pamoja
na washiriki wa Mkutano wa Kamati Kuu ya Utendaji ya WMO (WMO-Excecutive
Council-67) uliofanyika tarehe 15-17 Juni 2015, Geneva, Uswisi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Agnes Kijazi alikuwa miongoni mwa wajumbe 37
wa Mkutano wa Sitini na Saba wa Kamati Kuu ya Utendaji ya Shirika la Hali ya
Hewa Duniani (WMO-EC 67) uliofanyika makao makuu ya Shirika hilo kuanzia tarehe
15 hadi 17 Juni, 2015 Geneva nchini Uswisi. Kamati hiyo ina wajumbe 37
wanaowakilisha Nchi Wanachama wa WMO 191. Kati ya wajumbe hao tisa (9) wanatoka
Bara la Afrika na kati yao watano (5) ni wanawake wakiwemo wanawake wawili (2)
kutoka Bara la Afrika. Mkutano huo wa WMO-EC 67 ni wa kwanza kwa wajumbe wapya
waliochaguliwa wakati wa Mkutano Mkuu wa Kumi na Saba wa WMO (WMO-Congress-17) uliofanyika
kuanzia tarehe 25 Mei hadi 12 Juni 2015 ukihusisha wajumbe kutoka Nchi Wanachama
wa WMO.
Mkutano wa WMO-EC-67 pamoja na
masuala mengine ulijadili utekelezaji wa maazimio ya Mkutano Mkuu wa WMO ambayo
ni pamoja na uendelezaji Mpango Mkakati wa WMO (WMO Strategic Plan) ambao una
dira na vipaumbele vya WMO na Tasisi za Hali ya Hewa katika kipindi cha miaka minne ijayo (2016-2019).
Mpango Mkakati huu unajumuisha utekelezaji wa programu za utoaji wa huduma bora
zaidi za hali ya hewa kwa jamii “Global Framework for Climate Services (GFCS)”,
programu ya uboreshaji wa vituo vya upimaji wa hali ya hewa na ubadilishanaji
wa data za hali ya hewa “WMO Integrated Global Observing System and Information
System (WIGOS/WIS), utoaji wa tahadhari za mapema ili kukabiliana na maafa “High
impact services for disaster risk reduction”, Uboreshaji wa huduma za usalama
na usafiri wa anga “Aviation meteorological services”, uboreshaji wa huduma za
hali ya hewa kwa maeneo yenye barafu ya asili Duniani ikiwa ni pamoja na milima
mirefu kama Kilimanjaro “Polar and high mountain regions, Kujenga uwezo wa
rasilimali watu na vitendea kazi hasa kwa nchi zinazoendelea na visiwa vidogo
“Capacity Development” na masuala ya bajeti ya WMO na utawala bora kwa kipindi
cha 2015-2019. Maazimio makubwa yaliyofikiwa katika Mkutano huo ni kuhakikisha
wajumbe wote wanatimiza majukumu yao kwa weledi ili kuhakikisha huduma za hali
ya hewa duniani zinaboreshwa.
Dkt.
Agnes Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ambaye pia ni
mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), katika
picha na Wajumbe wa WMO-EC kutoka Afrika wakati wa Mkutano wa sitini na saba wa
Kamati Kuu ya Utendaji ya WMO, Geneva, Uswisi. Wa kwanza kulia kwake ni Dkt.
Amosi Makarau, Rais wa Afrika anayeshughulikia masuala ya Hali ya Hewa (RA-1);akifuatiwa
na Dkt. Linda Makuleni (Afrika ya Kusini), Dkt. Anthony Anuforom (Nigeria)
na Dkt. Mamadou Lamine Bah (Guinea); Wa kwanza kushoto kwake ni Bw. Fetene
Teshone (Ethiopia), akifuatiwa na Dkt. Daouda Konate (Ivory Coast). Wajumbe
wawili kutoka Afrika ambao ni Bw. Richard Philippe (Cameroon)
na Bw. Abdalah Mokssit (Morocco) ambaye pia ni Makamu wa Tatu wa Rais wa WMO
hawapo katika picha.
IMETOLEWA
NA: MONICA MUTONI-AFISA MAHUSIANO TMA
No comments:
Post a Comment