Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu Dkt Florence Turuku (wa tatu kutoka kushoto), Mwakilishi wa Shirika la
Hali ya Hewa Duniani (WMO) Mashariki na Kusini mwa Afrika (wanne kutoka
kushoto) Dkt Ellijah Mkhala, na Dkt.
Agnes Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TMA (wa pili kutoka kushoto) katika picha ya
pamoja kwenye kikao cha Kamati ya Taifa ya Maafa (TANDREC) kilichofanyika
tarehe 14 Agosti 2014.
Mamlaka ya Hali ya Hewa kwa kushirikiana na Shirika la Hali ya Hewa Duniani na Ofisi
ya Waziri Mkuu waliandaa kikao cha Kamati ya Maafa ya Taifa (TANDREC)
kuzungumzia utekelezaji wa GFCS hapa nchini. Mwenyekiti wa kikao hicho ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt.
Florence Turuku ambapo majadiliano yalijikita zaidi katika kuhakikisha
ushirikiano kati ya Kitengo cha Maafa nchini na GFCS. Kikao pia kiliweza
kupitia mapendekezo muhimu mawili; kwanza, Jukwaa la Kitaifa la Wadau wa Maafa
kuendelea kutumika katika kubadilishana mawazo na watumiaji na watoaji wa
huduma za hali ya hewa nchini. The meeting adopted two important recommendations; Pili, TANDREC itumike kama kamati
ya maendeleo ya GFCS.
Aidha, katika hotuba ya ufunguzi Dkt Turuku
alielezea umuhimu wa utekelezaji wa GFCS na kazi za kamati ya Taifa kusimamia
maendeleo ya GFCS nchini.
Dkt. Ellijah Mukhala, Mwakilishi wa
Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Mashariki na Kusini mwa Afrika, alielezea
kwa kifupi nia ya utekelezaji wa GFCS, ambao kwa hivi sasa umeanza kufanya kazi
kwa nchi za Tanzania na Malawi kwa udhamini wa Seriakali ya Norway. Alielezea
furaha yake kwa utekelezwaji wa GFCS kwa Tanzania mpaka hivi sasa imeundwa Timu
ya Mradi inayoongozwa na TMA, na mkutano wa wadau wa hali ya hewa uliojumuisha
zaidi ya wadau 60 kutoka kwa taaisi za serikali,taasisi zisizo za kiserikali,
wanahabari, katika mkutano huu mapendekezo mbalimbali yalitolewa yenye lengo la
kuboresha huduma za hali ya hewa nchini.
IMETOLEWA NA : MONICA MUTONI, OFISI YA UHUSIANO TMA
No comments:
Post a Comment