Tuesday, August 6, 2019

WIKI YA VIWANDA SADC: TMA YASISITIZA UMUHIMU WA MATUMIZI YA TAARIFA ZA HALI YA HEWA KATIKA UKUAJI WA SEKTA YA VIWANDA

Wataalam wa sayansi ya hali ya hewa wakitoa elimu kwa wananchi mbalimbali wanaotembelea banda la Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwenye maonesho ya wiki ya viwanda ya SADC, Ukumbi wa Julius Nyerere, Dar es Salaam
Wataalam wa sayansi ya hali ya hewa wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushiriki wa TMA na mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa kwa sasa  kwenye maonesho ya wiki ya viwanda ya SADC, Ukumbi wa Julius Nyerere, Dar es Salaam


Mamlaka ya Hali ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inashiriki maonesho ya 4 ya wiki ya viwanda SADC yanayoendelea katika viwanja vya ukumbi wa mwl. Nyerere, Dar es Salaam kuanzia tarehe 05 mpaka 09 Agosti 2019.
Katika maonesho hayo wananchi mbalimbali wameweza kupata elimu ya sayansi ya hali ya hewa katika kuchochea ukuaji wa sekta ya viwanda kwenye nchi za kusini mwa Afrika, ambapo wataalamu walipata fursa ya kuelezea umuhimu wa matumizi ya taarifa za hali ya hewa kwenye sekta zinachochea moja kwa moja ukuaji wa uchumi wa viwanda ikiwa na pamoja na upatikanaji wa malighafi,mitambo n.k.
Akizungumza na wananchi waliotembelea banda hilo, meneja wa huduma za hali ya hewa kwa usafiri wa anga na majini Bw. John Mayunga aliwaeleza wananchi jinsi usafiri wa anga na usafiri wa majini unavyoathirika na hali mbaya ya hewa hivyo kusisitiza kufuatilia na kufanya maamuzi stahiki taarifa hizo katika shughuli za usafirishaji.
Kwa upande wake Bw. Wilberforce Kikwasi mtabiri mwandamizi aliendelea kuwaasa wananchi kutumia fursa ya utabiri unaotolewa na TMA katika viwanja hivyo katika kufungasha bidhaa zao huku akitolea mfano wa mafuta ya mgando yaliyoyeyu kakutokana na joto la linaloendelea katika jiji la Dar es Salaam hususan muda wa mchana.
Katika maonesho hayo TMA imewaka ‘screen’ maalumu inayoonesha utabiri wa hali ya hewa kwa siku za 5 za maonesho hayo, hivyo kuweka fursa kwa washiriki na wananchi kwa ujumla kupata taarifa hizo sambamba na elimu.

No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...