Thursday, August 8, 2019

WIKI YA VIWADA SADC:NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA APONGEZA USAHIHI WA TAARIFA ZA HALI YA HEWA

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (MB) akimpa mkono wa pongezi Mkurugenzi wa huduma za utabiri-TMA Dkt. Hamza Kabelwa kwa niaba ya wafanyakazi wa TMA kwenye maonesho ya wiki ya viwanda ya SADC, Ukumbi wa Julius Nyerere, Dar es Salaam
Wataalamu wa hali ya hewa kutoka  TMA wakiendelea utoa elimu wa wageni  kwenye maonesho ya wiki ya viwanda ya SADC, Ukumbi wa Julius Nyerere, Dar es Salaam
Wataalamu wa hali ya hewa kutoka  TMA wakiendelea kutoa elimu kupitia vyombo vya habari kwenye maonesho ya wiki ya viwanda ya SADC, Ukumbi wa Julius Nyerere, Dar es Salaam
Wataalamu kutoka TMA katika picha ya pamoja kwenye maonesho ya wiki ya viwanda ya SADC, Ukumbi wa Julius Nyerere, Dar es Salaam



Tarehe 8/08/2019; Naibu waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara  Mhe. Mhandisi Stella M. Manyanya (MB) ameipongeza Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kazi nzuri inayoifanya kwa kutoa taarifa sahihi za hali ya hewa kwa wananchi.

Alizungumza hayo wakati alipotembelea banda la TMA katika Maonesho ya Wiki ya Viwanda ya SADC, viwanja vya ukumbi wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

‘Nawapongeza sana TMA kwa kazi nzuri mnayoifanya kwa sasa ya umakini ambao umehakikisha kiwango cha usahihi kimekuwa juu hivyo kutoa tabiri za kweli’

Aliongezea kwa kusema kutokana na usahihi huo, wizara ya viwanda imeweza kunufaika katika maendeleo ya ukuaji wa viwanda hususani upatikanaji wa malighafi za kilimo n.k

Kwa upande mwingine alitoa pongezi zake za dhati kwa Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi kwa kuchaguliwa kuwa Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani na hivyo kuiletea sifa nchi na kuwakilisha vyema wanawake wa Tanzania kimataifa


Alimalizia kwa kuwataka wafanyakazi wa TMA kuendelea kuchapa kazi kwa vile mchango wao unaonekana katika maendeleoya nchi


No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...