Tuesday, October 5, 2021

WATANZANIA WAASWA KUCHANGAMKIA FURSA MBALIMBALI ZITAKAZOJITOKEZA KWA KUJIUNGA NA “AMCOMET”

Mgeni rasmi Ndg. Amour Hamil Bakari ambaye pia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, akizungumza na washiriki wakati akifungua rasmi kikao cha kupata maoni ya wadau kuhusiana na mapendekezo ya kusaini Katiba ya Baraza la Mawaziri wenye dhamana ya Hali ya Hewa katika Bara la Afrika, yaani 'African Ministerial Conference on Meteorology (AMCOMET)' kilichofanyika Tarehe 04 Oktoba 2021 katika ukumbi wa Jengo la malaria, Mwanakwerekwe - Zanzibar.

Muwakilishi wa Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) (SMT) Ndg. Biseko Paul Chiganga, akisisitiza jambo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzungumza na washiriki wa kikao cha kupata maoni ya wadau kuhusiana na mapendekezo ya kusaini Katiba ya Baraza la Mawaziri wenye dhamana ya Hali ya Hewa katika Bara la Afrika, yaani 'African Ministerial Conference on Meteorology (AMCOMET)' kilichofanyika Tarehe 04 Oktoba 2021 katika ukumbi wa Jengo la malaria, Mwanakwerekwe - Zanzibar.

Muwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Ndg. Mohammed Ngwali, akitoa neno la shukurani kwa mgeni rasmi katika kikao cha kupata maoni ya wadau kuhusiana na mapendekezo ya kusaini Katiba ya Baraza la Mawaziri wenye dhamana ya Hali ya Hewa katika Bara la Afrika, yaani 'African Ministerial Conference on Meteorology (AMCOMET)' kilichofanyika Tarehe 04 Oktoba 2021 katika ukumbi wa Jengo la malaria, Mwanakwerekwe - Zanzibar.




Washiriki wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi katika kikao cha kupata maoni ya wadau kuhusiana na mapendekezo ya kusaini Katiba ya Baraza la Mawaziri wenye dhamana ya Hali ya Hewa katika Bara la Afrika, yaani 'African Ministerial Conference on Meteorology (AMCOMET)' kilichofanyika Tarehe 04 Oktoba 2021 katika ukumbi wa Jengo la malaria, Mwanakwerekwe - Zanzibar.












Washiriki mbalimbali wakichangia mada katika kikao cha kupata maoni ya wadau kuhusiana na mapendekezo ya kusaini Katiba ya Baraza la Mawaziri wenye dhamana ya Hali ya Hewa katika Bara la Afrika, yaani 'African Ministerial Conference on Meteorology (AMCOMET)' kilichofanyika Tarehe 04 Oktoba 2021 katika ukumbi wa Jengo la malaria, Mwanakwerekwe - Zanzibar.

Mgeni rasmi (katikati ya walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao cha kupata maoni ya wadau kuhusiana na mapendekezo ya kusaini Katiba ya Baraza la Mawaziri wenye dhamana ya Hali ya Hewa katika Bara la Afrika, yaani 'African Ministerial Conference on Meteorology (AMCOMET)' kilichofanyika Tarehe 04 Oktoba 2021 katika ukumbi wa Jengo la malaria, Mwanakwerekwe - Zanzibar.

 

Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Ndg. Amour Hamil Bakari, amewaasa Watanzania kuchangamkia fursa mbalimbali zitakazojitokeza baada ya Tanzania kujiunga na “AMCOMET”. Aliyasema hayo alipokuwa akifungua rasmi kikao cha kupata maoni ya wadau kuhusiana na mapendekezo ya kusaini Katiba ya Baraza la Mawaziri wenye dhamana ya Hali ya Hewa katika Bara la Afrika, yaani “African Ministerial Conference on Meteorology (AMCOMET)”

“Naomba nitumie fursa hii kupitia ufunguzi wa kikao hiki cha kupata maoni ya mapendekezo ya kusaini katiba ya Baraza la Mawaziri wenye dhamana ya Hali ya Hewa - Barani Afrika, kuwaasa Watanzania kutumia fursa mbalimbali zikiwemo za ajira zitakazojitokeza baada ya kujiunga na “AMCOMET”.” alisema Katibu Mkuu Amour Hamil Bakari.

Aidha, Ndg. Bakari aliongezea kuwa uchumi wa nchi yetu pamoja na nchi zingine zinazotuzunguka unategemea zaidi sekta za kiuchumi na kijamii ambazo hutegemea na kuathiriwa sana na hali ya hewa, hususan kwa kuzingatia kuwa hali ya hewa haitambui mipaka ya kijiografia, hivyo nchi zinazofanana katika mifumo ya hali ya hewa zimekuwa na programu za pamoja za kikanda na kimataifa ili kupata suluhisho la kupunguza athari za majanga yatokanayo na hali mbaya ya hewa na mabadiliko ya hali ya hewa.

Muwakilishi wa Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) (SMT) Ndg. Biseko Paul Chiganga, alisisitiza kuendelea kuimarisha ushirikiano katika masuala ya muungano baina ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (SMT) pamoja na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi (SMZ), ukilenga kuweka uelewa wa pamoja na baadae kutatua changamoto mbalimbali baina ya sekta za hali ya hewa na usafiri wa anga na sekta nyingine mtambuka.

Aidha, Muwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Ndg. Mohammed Ngwali, alimshukuru mgeni rasmi kwa kukubali kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa kikao hicho muhimu cha kupokea maoni ya wadau kitakachoiwezesha Tanzania kupiga hatua zaidi katika mchakato wa kusaini katiba ya “AMCOMET”.

TMA YAKUTANA NA WADAU WA MADINI KUJENGA UELEWA WA UTEKELEZAJI WA KANUNI ZA SHERIA NA.2 YA 2019 YA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Mgeni rasmi ambaye ni mwakilishi wa Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) Bw. Hamid Mbegu (katikati) katika picha ya pamoja na wachimbaji wakubwa, wawakilishi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), wawakilishi wa Tume ya Madini na wataalam kutoka TMA katika Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Madini kuhusu kujenga uelewa wa pamoja wa utekelezaji wa kanuni za sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Na.2 ya mwaka 2019.








Mgeni rasmi ambaye ni mwakilishi wa Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) Bw. Hamid Mbegu (katikati) katika picha ya pamoja na wachimbaji wa kati, wawakilishi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), wawakilishi wa Tume ya Madini na wataalam kutoka TMA katika Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Madini kuhusu kujenga uelewa wa pamoja wa utekelezaji wa kanuni za sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Na.2 ya mwaka 2019.






Dodoma; Tarehe 29 – 30 Septemba, 2021; 

TMA imekutana na wadau wa sekta ya madini nchini ili kujenga uelewa wa pamoja wa utekelezaji wa Kanuni za Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Na.2 ya 2019. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa PSSSF (Makale), Dodoma, Tarehe 29 - 30 Septemba 2021. Akizungumza wakati akifungua mkutano wa Wadau wa Madini mgeni rasmi, ambaye ni mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) Bw. Hamid Mbegu alisema kanuni hizo zimekamilika na zipo tayari kwa utekelezaji. 

 “Wizara kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imekamilisha kanuni saba za sheria Na.2 ya 2019. Utekelezaji wa kanuni hizi katika sekta ya madini utasaidia kupunguza madhara yanayotokana na matukio ya hali ya hewa migodini kupitia matumizi ya taarifa mahsusi na sahihi za hali ya hewa”. Alizungumza Bw. Mbegu. 

 Aidha, Bw. Mbegu alisema TMA imeandaa mifumo ya kufungasha na kufikisha huduma kwa wadau wa sekta ya madini sambamba na mfumo wa kusajili vituo vya hali ya hewa nchini kwa kuzingatia masharti ya kanuni juu ya uwekaji na uendeshaji wa vituo vya hali ya hewa ili kupata takwimu sahihi kwa matumizi mapana ya sekta ya hali ya hewa na wadau wake. 

 Awali, wakati akimkaribisha mgeni rasmi, Dkt. Agnes Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) alieleza jukumu la Mamlaka ya Hali ya Hewa na umuhimu wa kikao hicho cha wadau wa madini.

 “Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ina jukumu la kuhakikisha inatoa huduma za hali ya hewa zilizo bora kwa wadau mbalimbali ikiwepo sekta ya madini. Hivyo, kikao hiki ni muhimu kwasababu kitagusa maeneo mawili muhimu ya kisheria na tayari yapo katika kanuni, ambayo ni umiliki wa vituo vya hali ya hewa na uchangiaji wa huduma za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa katika sekta ya madini nchini”. Alisema Dkt. Kijazi. 

Kwa upande wa wadau, waliishukuru TMA kwa ushirikishwaji wa mkutano huu wa kujenga uelewa wa pamoja wa utekelezaji wa kanuni za Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Na.2 ya 2019 na kusema matumizi ya taarifa za hali ya hewa katika sekta ya madini ni muhimu hivyo Mamlaka itoe elimu zaidi ili kupata uelewa wa pamoja kwa wadau wote. 

Naye, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Adv. Mohamed Salum akizungumza wakati wa kufunga mkutano huo, aliwashukuru wadau wa sekta ya madini kwa kushiriki mkutano huo wa kujenga uelewa wa utekelezaji wa kanuni za TMA zilizokuwa chini ya Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Na.2 ya 2019 na kukiri kuwa wadau wameonesha uelewa mkubwa na umuhimu juu ya utekelezaji wa sheria hii na namna itakavyowasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ya uchimbaji wa madini na kuonesha kwamba uhitaji wa taarifa za hali ya hewa ni jambo la muhimu kabla ya kuanza shughuli zao. 


IMETOLEWA NA: 
KITENGO CHA UHUSIANO 
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA (TMA) 

 

MHE. WAITARA AMEITAKA TMA KUWEKEZA KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA CHUO CHA HALI YA HEWA.


Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi(Sekta ya Uchukuzi), Mhe. Mwita Mwikwabe Waitara (MB) (katikati) akiongea na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania wakati wa ziara yake,  akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Dkt. Buruhani Nyenzi (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani, Dkt. Agnes Kijazi (Kulia).

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi(Sekta ya Uchukuzi), Mhe. Mwita Mwikwabe Waitara (MB) (katikati)   akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Dkt. Buruhani Nyenzi (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani, Dkt. Agnes Kijazi (Kushoto) na Menejiment ya TMA.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi(Sekta ya Uchukuzi), Mhe. Mwita Mwikwabe Waitara (MB) (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi, Dkt. Ladislaus Chang'a (wa pili kulia) wakati wa ziara yake.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi(Sekta ya Uchukuzi), Mhe. Mwita Mwikwabe Waitara (MB)(kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani, Dkt. Agnes Kijazi (kulia)kuhusu takwimu mbali mbali ya hali ya hewa zinavyohifadhiwa.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi(Sekta ya Uchukuzi), Mhe. Mwita Mwikwabe Waitara (MB) (kulis) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Huduma za Utabiti, Dit. Hamza Kabelwa (kushoto).


Dar es Salaam; Tarehe 04 Oktoba, 2021;

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi(Sekta ya Uchukuzi), Mhe. Mwita Mwikwabe Waitara (MB) ameitaka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuwekeza zaidi katika kuboresha mazingira ya chuo cha hali ya hewa kilichopo Kigoma.

Hayo yalizungumzwa katika ziara ya Mhe. Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi iliyofanyika katika ofisi za Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Ubungo Plaza, Tarehe 04/10/2021. Lengo la ziara hiyo ni kuifahamu TMA, kazi wanazofanya na kutambua changamoto za kiutendaji ili kuweza kufanya maboresho stahiki. 

“Nilipokwenda Chuo cha hali ya hewa Kigoma niliona mazingira yake sio mazuri pamoja na kuwa Chuo hicho kipo katika ukarabati kinahitaji kiwe na mazingira mazuri kutokana na kuwa ndio chou pekee kinachotoa mafunzo ya awali ya hali ya hewa hapa nchini. Nafikiri mwenyekiti wa bodi na Mkurugenzi Mkuu mnapaswa kuwekeza pale” Alizungumza Mhe. Waitara.

Mheshimiwa Naibu Waziri aliongezea kuwa Mamlaka inajukumu kubwa kwasababu taarifa za hali ya hewa zinatumika katika sekta zote za maendeleo hapa nchini.  Mwekezaji akitaka kuwekeza lazima afuatilie taarifa za hali ya hewa ili kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Aidha aliwapongeza TMA kwa kazi nzuri wanazozifanya na kuwataka waendelee kufanya kazi kwa weledi wakijua kwamba kazi wanazozifanya zina mchango mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii hapa nchini. “Nawapongeza kwa kuboresha huduma za hali ya hewa hapa nchini na pia kuifanya Tanzania iendelee kung’ara katika Nyanja za kimataifa kwenye sekta ya hali ya hewa. Aliongeza Mhe. Waitara.

Mhe. Waitara aliahidi kwamba katika utaratibu wa kuboresha maslahi ya watumishi kama alivyoahidi Mhe. Rais watumishi wa TMA wataboreshewa Maslahi yao ili waweze kufanyakazi kwa ufanisi. 

Awali, wakati akimkaribisha Mhe. Naibu Waziri, Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Dkt. Buruhani Nyenzi kupitia taarifa yake fupi alisema kuwa Mamlaka imeanza kuifanyia kazi changamoto ya vifaa ambapo Serikali imeendelea kutenga fedha kwaajili ya ununuzi wa vifaa vya hali ya hewa. Changamoto ya maslahi duni nayo pia imeanza kufanyiwa kazi ambapo ‘Job Evaluation’ imefanyika kwa kutumia Chuo cha Utumishi wa Umma na mapendekezo ya mishahara stahiki kwa wafanyakazi yamewasilishwa katika Mamlaka husika. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani, Dkt. Agnes Kijazi alishukuru Serikali, “Napenda kuishukuru Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwani imeendelea kuiwezesha Mamlaka kuwa na vitendea kazi vya kisasa na wataalamu bingwa ambao wanapatiwa mafunzo mara kwa mara kwa lengo la kuwaongeza ujuzi”. Alisema Dkt. Kijazi. Aliongeza kusema “Nichukue fursa hii adhimu kuishukuru Serikali yetu kupitia Wizara kwa kutupatia Rada nyingine mbili ambazo ukamilikaji wake utapelekea kufikiwa kwa malengo ya muda mrefu ya kuwa na Rada 7 za hali ya hewa kwa nchi nzima”.

 

Alimalizia kwa kumhakikisha Mhe. Naibu Waziri kwamba maelekezo yote aliyoyatoa hususani uboreshaji wa Miundombinu ya Chuo cha Hali ya Hewa Kigoma yatawekewa mpango mkakati wa utekelezaji.

 

Thursday, September 23, 2021

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA (TMA) YAPATA VIFAA VIPYA VYA KUPIMA HALI YA HEWA YA ANGA LA JUU (UPPER AIR)

Wataalamu wa hali ya hewa kituo cha TMA-JNIA, wakifuatilia mafunzo ya uendeshaji wa mtambo mpya waupimaji wa hali ya hewa ya anga la juu. Mafunzo yalitolewa na mkufunzi kutoka kampuni ya MODEM ya Nchini Ufaransa, Bw. Benjamin Finot, tarehe 8 Septemba, 2021.



 Wataalamu wa hali ya hewa wakiwa katika mafunzo kwa vitendo ya urushaji puto linalobeba kifaa cha radiosonde kinachopima haliya hewa ya anga la juu, baada ya kukamilika zoezi la kufungwa vifaa hivyo JNIA, tarehe 8 Septemba, 2021



Dar es Salaam; Tarehe 13/09/2021

Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) limeipatia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)vifaa vipya vya kupima hali ya hewa ya anga la juu (upper air).Vifaa hivyo vimetolewa kwa TMA ikiwa ni msaada chini ya utekelezaji wa program ya WMO ya kuboresha huduma za hali ya hewa kwa Nchi Wanachama wa Afrika Mashariki (EAC) zinazozunguka eneo la Ziwa Viktoria, iitwayo “HIGH impact Weather lAke SYstems (HIGHWAY)”.

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na: mtambo wa kuzalisha gesi ya haidrojeni (Hydrogen gas Generator); radiosonde; Maputo maalumu ya kupima hali ya hewa ya anga za juu (weather balloons);program za kompyuta (computer softwares)na mavazi maalumu kwa ajili ya usalama. Vifaa hivyo vimefungwa tarehe 7 Septemba, 2021 katika kituo cha kupima hali ya hewa ya anga la juu (Upper Air Station) kilichopo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa MwalimuJulius Nyerere, Dar es Salaam (JNIA). Aidha, zoezi la ufungaji wa vifaa hivyo lilienda sambamba na mafunzo kwa wataalamu.

Ufungwaji wa vifaa hivyo umewezesha kuhuisha kituo hichokuwa cha kisasa zaidi baada ya mitambo ya awali kuwa chakavu. Kituo hicho kwa sasa kitaendelea na shughuli zake za kupima hali ya hewa ya anga la juu kama kawaida.Uhuishaji wakituo hicho utawezesha kupima takwimu za hali ya hewa ya anga la juu, ambazo ni muhimu sana katikakutoa utabiri wa hali ya hewa kwa matumizi mbalimbali hususan usalama na usafiri wa anga nchini. 

Programu hiyo ya HIGHWAY ilitekelezwa nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano, kuanzia Septemba, 2017, ambapo miongoni mwa shughuli zake zilihusisha pia uhuishaji wa kituo hicho cha kupima hali ya hewa ya anga la juu katika uwanja wa JNIA. Msaada wa vifaa vilivyotolewa na WMO  ni sehemu ya utaratibu wa Shirika hilo ikiwa ni mrejesho kwa Nchi Wanachama kutokana na michango inayotolewa na Serikali za Nchi Wanachama kupitia ada ya uanachama kwa Shirika hilo.

Thursday, September 16, 2021

ZIARA YA MHE. NAIBU WAZIRI KATIKA OFISI ZA TMA -MWANZA


Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Mwita Waitara (MB) akipata maelezo kuhusiana na utoaji huduma Bora za hali ya hewa kwa usafiri wa anga katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza. Tarehe 16/09/2021.




 

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...