Sunday, December 7, 2014

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA (TMA) NA OFISI YA HALI YA HEWA YA UINGEREZA (UK MET OFFICE) WASAINI MKATABA WA MAKUBALIANO (MoU) YA USHIRIKIANO KATIKA KUBORESHA HUDUMA ZA HALI YA HEWA NCHINI





Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa,  Dkt. Agnes Kijazi akisaini mkataba  na mtendaji mkuu wa  Ofisi ya Hali ya Hewa ya Uingereza Dkt. Rob Varley. Tukio hilo lilishuhudiwa na Dkt. Ladislaus Chang’a, Mkurugenzi wa Utafiti katika Mamlaka ya Hali ya Hewa na Bi. Jane Wardle mtaalam wa masuala ya hali ya hewa kutoka ofisi ya hali ya hewa ya Uingereza.


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Ofisi ya Hali ya Hewa ya Uingereza (UK Met Office) wamesaini mkataba wa makubaliano ya uboreshaji huduma za hali ya hewa hapa  nchini.  Mkataba huo umesainiwa  tarehe 11 Novemba, 2014 wakati wa kikao cha masuala ya hali ya hewa (IBCS) kilichofanyika  mjini Geneva Uswiss. 

Akizungumzia makubaliano hayo Dkt Agnes Kijazi alisema Mamlaka ya Hali ya Hewa ililiomba Shirika la Hali ya Hewa Duniani kuisaidia TMA kuboresha huduma zake ili ziwe za kisasa (Modernization of meteorological services in Tanzania) na ofisi ya hali ya hewa ya Uingereza ilikubali kuisaidia TMA katika zoezi hilo. ‘Makubaliano tunayosaini leo ni sehemu tu ya kazi kubwa ya uboreshaji wa huduma za hali ya hewa nchini ambapo shirika  la Kimataifa la Uingereza (DFID) kupitia Ofisi ya Hali ya Hewa ya Uingereza limeipatia TMA Pound 70,000’ alisema Dkt. Kijazi .  Akifafanua  kuhusu matumizi ya fedha hizo Dkt. Kijazi alisema fedha hizo zitatumika  kuijengea uwezo TMA kutunza  data za hali ya hewa za kihistoria kwa njia ya digitali na pia kuwajengea uwezo watumishi wa TMA kutoa huduma bora zinazokidhi matarajio ya wadau na hivyo kulinda maisha ya watu na  mali zao.  

Kwa upande wake mkuu wa Ofisi ya Hali ya Hewa ya Uingereza  Dkt. Rob Varley alisema anafurahia ushirikiano uliopo kati ya TMA na UK met office na akaahidi kuendeleza ushirikiano huo na pia kuisadia TMA kuboresha huduma zake.
Imetolewa na : Monica Mutoni Afisa Mahusiano -TMA

Saturday, November 29, 2014

HALI YA HEWA YAENDELEA KUWANOA WATAALAMU WAKE KATIKA KUKIDHI VIWANGO VYA SHIRIKA LA HALI YA HEWA DUNIANI (WMO)




Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi ambaye pia alikuwa mgeni rasmi akizungumza na wahitimu wa mafunzo ya huduma za hali ya hewa kwa ajili ya usafiri wa anga kutoka Chuo cha Hali ya Hewa Kigoma



Mwakilishi wa wahitimu Bi. Pamela Levira akisoma risala ya wahitimu kwa mgeni rasmi katika mahafali ya pili ya mafunzo ya huduma za hali ya hewa kwa ajili ya usafiri wa anga kutoka Chuo cha Hali ya Hewa Kigoma

Mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi katika picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo ya huduma za hali ya hewa kwa ajili ya usafiri wa anga kutoka Chuo cha Hali ya Hewa Kigoma,Kulia kwake mwenye tai nyekundu ni Mkuu wa Chuo cha Hali ya Hewa Kigoma Bw. Joseph Aliba


Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini iliendesha mafunzo ya hali ya hewa kwaajili ya usafiri wa anga ‘Aeronautical Meteorology’. Mafunzo haya yalikuwa yakiendeshwa chini ya Chuo cha Hali ya Hewa Kigoma ikiwa ni kuhakikisha wafanyakazi wa Mamlaka ya hali ya Hewa (TMA) kwa upande wa huduma za hali ya hewa kwa usafiri wa anga wanakidhi vigezo vilivyowekwa na WMO. Mafunzo haya ni ya pili kutolewa hapa nchini kupitia Chuo cha Hali ya Hewa Kigoma.
Akifunga mafunzo hayo, Mgeni rasmi katika mahafali ya pili ya Kozi ya Hali ya Hewa kwa ajili ua Usafiri wa Anga; Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt Agnes Kijazi alimpongeza Mkuu wa Chuo kwa kufanikisha kuendesha mafunzo hayo kwa mara ya pili ambayo ni moja ya utekelezaji wa vigezo vilivyowekwa kimataifa na WMO. ‘Kuendesha mafunzo haya kutawezesha Mamlaka kuwa na wataalamu wa kutosha wanaokubalika kimataifa kutoa huduma za hali ya hewa kwaajili ya usafiri wa anga, hivyo Mamlaka itakuwa imefikia viwango vilivyowekwa na Shirika la Hali ya Hewa Duniani, vinavyozitaka taasisi za hali ya hewa duniani kuwa na na wataalamu wenye shahada ya hali ya hewa na ujuzi unaotakiwa kwaajili ya kutoa huduma katika usafiri wa anga’Alisema Dk. Kijazi. Aidha aliwataka wahitimu kutumia ujuzi waliopata ili kufanya kazi kwa ufanisi na hviyo kuchangia katika maendeleo ya taifa.
Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha hali ya hewa Kigoma Bwana Joseph Aliba alisema Chuo cha Hali ya Hewa Kigoma kimepata usajili wa kudumu toka NACTE na waalimu wote wamesajiliwa na NACTE.
Akiongea kwa niaba ya wahitimu Bi Pamela Levira ameishukuru Mamlaka kwa kuwajengea uwezo  wa kufanya kazi kwa kujiamini katika kutoa huduma za hali hewa katika sekta ya usafiri wa anga.
Chuo cha Hali ya Hewa Kigoma  ni chuo pekee Tanzania kinachotoa elimu ya ngazi ya cheti na diploma kwa taalamu ya hali ya hewa. Chuo kimepata usajili wa NACTE kwa leseni ya kuendesha mafunzo ya nje ya mipaka ya nchi ‘cross boarder license’.
Imetolewa na : Monica Mutoni Ofisa Uhusiano- Mamlaka ya Hali ya Hewa

TANZANIA METEOROLOGICAL AGENCY CONTINUES TO BUILD EMPLOYEE’S CAPACITY TO MEET WORLD METEOROLOGICAL ORGANIZATION (WMO) REQUIREMENTS







TMA has conducted a second short course in Aviation Meteorology for Meteorologists to ensure that the standard required by WMO is met. This training was facilitated by Kigoma National Meteorological Training Centre (KNMTC).
The Director General of TMA, Dr Agnes Kijazi, congratulated the Management of KNMTC, during the graduation ceremony held on 28th November 2014, for facilitating the training for the second time. “Conducting this training will enable Meteorologists to meet WMO requirements on Aviation Meteorology.’’, says Dr Agnes Kijazi. The participants were also asked to utilize the knowledge gained to excel in their daily aviation duties.
Speaking on behalf of graduates Ms  Pamela, appreciate the effort done by TMA to ensure staff competence on provision of aeronautical services.
Kigoma National Meteorological Training Centre is the only centre in Tanzania which is able to provide a Meteorological Certificate and Diploma level. The Centre is registered under NACTE and also has a cross border license. It is planning to extend its training both in Tanzania and internationally.  
Issued by: Monica Mutoni, TMA Public Relation Office.

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...