Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa, Dkt. Agnes Kijazi akisaini mkataba na mtendaji mkuu wa Ofisi ya Hali ya Hewa ya Uingereza Dkt. Rob
Varley. Tukio hilo lilishuhudiwa na Dkt. Ladislaus Chang’a, Mkurugenzi wa
Utafiti katika Mamlaka ya Hali ya Hewa na Bi. Jane Wardle mtaalam wa masuala ya
hali ya hewa kutoka ofisi ya hali ya hewa ya Uingereza.
Mamlaka
ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Ofisi ya Hali ya Hewa ya Uingereza (UK Met
Office) wamesaini mkataba wa makubaliano ya uboreshaji huduma za hali ya hewa
hapa nchini. Mkataba huo umesainiwa tarehe 11 Novemba, 2014 wakati wa kikao cha
masuala ya hali ya hewa (IBCS) kilichofanyika mjini Geneva Uswiss.
Akizungumzia
makubaliano hayo Dkt Agnes Kijazi alisema Mamlaka ya Hali ya Hewa ililiomba
Shirika la Hali ya Hewa Duniani kuisaidia TMA kuboresha huduma zake ili ziwe za
kisasa (Modernization of meteorological services in Tanzania) na ofisi ya hali
ya hewa ya Uingereza ilikubali kuisaidia TMA katika zoezi hilo. ‘Makubaliano
tunayosaini leo ni sehemu tu ya kazi kubwa ya uboreshaji wa huduma za hali ya
hewa nchini ambapo shirika la Kimataifa
la Uingereza (DFID) kupitia Ofisi ya Hali ya Hewa ya Uingereza limeipatia TMA
Pound 70,000’ alisema Dkt. Kijazi . Akifafanua
kuhusu matumizi ya fedha hizo Dkt. Kijazi alisema fedha hizo zitatumika kuijengea uwezo TMA kutunza data za hali ya hewa za kihistoria kwa njia
ya digitali na pia kuwajengea uwezo watumishi wa TMA kutoa huduma bora zinazokidhi matarajio ya wadau na hivyo
kulinda maisha ya watu na mali zao.
Kwa upande wake mkuu wa Ofisi ya Hali ya Hewa ya
Uingereza Dkt. Rob Varley alisema
anafurahia ushirikiano uliopo kati ya TMA na UK met office na akaahidi
kuendeleza ushirikiano huo na pia kuisadia TMA kuboresha huduma zake.
Imetolewa na : Monica Mutoni Afisa Mahusiano -TMA
No comments:
Post a Comment