Mkurugenzi Mkuu
wa TMA Dkt. Agnes Kijazi ambaye pia alikuwa mgeni rasmi akizungumza na wahitimu
wa mafunzo ya huduma za hali ya hewa kwa ajili ya usafiri wa anga kutoka Chuo
cha Hali ya Hewa Kigoma
Mwakilishi wa
wahitimu Bi. Pamela Levira akisoma risala ya wahitimu kwa mgeni rasmi katika
mahafali ya pili ya mafunzo ya huduma za hali ya hewa kwa ajili ya usafiri wa
anga kutoka Chuo cha Hali ya Hewa Kigoma
Mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes
Kijazi katika picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo ya huduma za hali ya hewa
kwa ajili ya usafiri wa anga kutoka Chuo cha Hali ya Hewa Kigoma,Kulia kwake
mwenye tai nyekundu ni Mkuu wa Chuo cha Hali ya Hewa Kigoma Bw. Joseph Aliba
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini iliendesha
mafunzo ya hali ya hewa kwaajili ya usafiri wa anga ‘Aeronautical Meteorology’.
Mafunzo haya yalikuwa yakiendeshwa chini ya Chuo cha Hali ya Hewa Kigoma ikiwa
ni kuhakikisha wafanyakazi wa Mamlaka ya hali ya Hewa (TMA) kwa upande wa
huduma za hali ya hewa kwa usafiri wa anga wanakidhi vigezo vilivyowekwa na
WMO. Mafunzo haya ni ya pili kutolewa hapa nchini kupitia Chuo cha Hali ya Hewa
Kigoma.
Akifunga mafunzo hayo, Mgeni rasmi katika
mahafali ya pili ya Kozi ya Hali ya Hewa kwa ajili ua Usafiri wa Anga;
Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt Agnes Kijazi alimpongeza Mkuu wa Chuo kwa
kufanikisha kuendesha mafunzo hayo kwa mara ya pili ambayo ni moja ya
utekelezaji wa vigezo vilivyowekwa kimataifa na WMO. ‘Kuendesha mafunzo haya
kutawezesha Mamlaka kuwa na wataalamu wa kutosha wanaokubalika kimataifa kutoa
huduma za hali ya hewa kwaajili ya usafiri wa anga, hivyo Mamlaka itakuwa imefikia
viwango vilivyowekwa na Shirika la Hali ya Hewa Duniani, vinavyozitaka taasisi
za hali ya hewa duniani kuwa na na wataalamu wenye shahada ya hali ya hewa na
ujuzi unaotakiwa kwaajili ya kutoa huduma katika usafiri wa anga’Alisema Dk.
Kijazi. Aidha aliwataka wahitimu kutumia ujuzi waliopata ili
kufanya kazi kwa ufanisi na hviyo kuchangia katika maendeleo ya taifa.
Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha hali ya hewa
Kigoma Bwana Joseph Aliba alisema Chuo cha Hali ya Hewa Kigoma kimepata usajili
wa kudumu toka NACTE na waalimu wote wamesajiliwa na NACTE.
Akiongea kwa niaba ya wahitimu Bi Pamela
Levira ameishukuru Mamlaka kwa kuwajengea uwezo
wa kufanya kazi kwa kujiamini katika kutoa huduma za hali hewa katika
sekta ya usafiri wa anga.
Chuo cha Hali ya Hewa Kigoma ni chuo pekee Tanzania kinachotoa elimu ya
ngazi ya cheti na diploma kwa taalamu ya hali ya hewa. Chuo kimepata usajili wa
NACTE kwa leseni ya kuendesha mafunzo ya nje ya mipaka ya nchi ‘cross boarder
license’.
Imetolewa na : Monica
Mutoni Ofisa Uhusiano- Mamlaka ya Hali ya Hewa
No comments:
Post a Comment