Mamia ya wanafunzia wa shule za msingi na sekondari wametembelea banda la Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) katika maonesho ya Nane Nane 2023, Morogoro, Kanda ya Mashariki ili kupata elimu ya sayansi ya hali ya hewa ikiwemo vifaa vya kisasa, matumizi ya taarifa za hali ya hewa na athari za mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi.
Wakizungumza wakati wa ziara zao katika nyakati tofauti, Mwalimu Mgata kutoka Shule ya Msingi Agape, alisema wanafunzi wake wameweza kiujifunza kuhusu vifaa vya kisasa na namna utabiri unaweza kutabiriwa kwa muda mfupi.
Aidha, Mwalimu Sadam Said kutoka Shule ya Sekondari Green City alieleza kuwa kupitia ziara yao, wameweza kujifunza kwa vitendo ambapo darasani wamekuwa wakifundisha kwa nadharia, hivyo kutoa uelewa mkubwa zaidi.
Kwa upande wao wa wakilishi wa wanafunzi, walieleza jinsi alivyojifunza namna ya kuandaa utabiri kisayansi na kisasa kwa kutumia njia mbalimbnali ikiwemo satelaiti na rada.
No comments:
Post a Comment