Monday, August 7, 2023

HUDUMA MAHUSUSI NEEMA KWA WAKULIMA


 Mbeya; Tarehe 03 Agosti, 2023;

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inashiriki katika maonesho ya NaneNane yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale, Uyole – Mbeya, kuanzia tarehe 1 hadi 8 Agosti 2023. Kupitia maonesho hayo Meneja wa Huduma za Hali ya Hewa Kilimo, Ndg. Isack Yonah amezungumza na wananchi kupitia vyombo mbalimbali vya habari akiwakaribisha wakulima kufika bandani hapo ili kupata elimu ya hali ya hewa pamoja na kufahamu umuhimu wa kutumia huduma mahususi katika maeneo yao.

“ Magonjwa mengi yanayoshambulia mazao yatategemea hali ya hewa, pia hali ya baridi husababisha mazao kuchelewa kukomaa, lakini sasa kupitia huduma hizi mahususi itakuwa neema kwa mkulima kwa sababu tutamfungashia kadri anavyohitaji yeye ili apange namna ya kukabiliana na hali tarajiwa katika eneo alilopo” alisisitiza Ndg. Isack Yonah.

Aidha, Kaimu Meneja Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi -TMA Songwe, Ndg. Abel Nyamenda ameelezea kuwa kwa sasa TMA inatumia teknolojia ipasavyo katika kutoa huduma bora kwa wateja wake, hivyo ni vyema wadau kuzitumia huduma hizo ili kuleta tija katika sekta zao.

Kwa upande mwingine wananchi waliotembelea bandani hapo waliomba Mamlaka kujenga ofisi zao huko vijijini ili mkulima anapohitaji huduma hizo mahususi iwe rahisi kuzipata kwa wakati zikiwa sahihi ili kuepusha kuwekeza katika kilimo na kupata hasara.


No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...