|
Wajumbe wa Bodi mpya ya TMA katika picha ya pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi.Isack Kamwelwe wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo |
|
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi. Isack Kamwelwe akizungumza na wajumbe wa Bodi katika hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo. |
|
Mwenyekiti wa Bodi mpya ya TMA Dkt. Buruhani Nyenzi akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo. |
|
Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa WMO, akitoa taarifa fupi ya TMA wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo. |
|
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi. Isack Kamwelwe akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya TMA Dkt. Buruhani Nyenzi, nyenzo muhimu za utendaji kazi katika hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo. |
|
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi. Isack Kamwelwe
akimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TMA Dkt. Makame Omar Makame, nyenzo
muhimu za utendaji kazi katika hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo. |
|
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi. Isack Kamwelwe
akimkabidhi Katibu wa Bodi ya TMA Dkt. Agnes Kijazi, nyenzo
muhimu za utendaji kazi katika hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo. |
|
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi. Isack Kamwelwe
akimkabidhi Mjumbe wa Bodi ya TMA Mhandisi. Aron Kisaka, nyenzo
muhimu za utendaji kazi katika hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo. |
|
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi. Isack Kamwelwe
akimkabidhi Mjumbe wa Bodi ya TMA Bi. Marystella Mtalo, nyenzo
muhimu za utendaji kazi katika hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo. |
|
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi. Isack Kamwelwe
akimkabidhi Mjumbe wa Bodi ya TMA Kapt. Large Temba, nyenzo
muhimu za utendaji kazi katika hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo. |
|
Wajumbe wa Menejimenti ya Mamlaka katika picha ya pamoja na Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi.Isack Kamwelwe wakati wa
hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo |
Dar es
Salaam, Tarehe 28/11/2019: “Mkasimamie vizuri jukumu jipya
la Mamlaka la usimamizi wa huduma za hali ya hewa nchini kama ilivyoainishwa
katika sheria”. Alizungumza Mhe. Mhandisi. Isack Kamwelwe, Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, wakati akizindua rasmi Bodi mpya ya Mamlaka ya Hali ya
Hewa Tanzania (TMA).
Mhe. Kamwelwe aliitaka Bodi hiyo kuhakikisha kuwa
inasimamia kwa umakini utekelezaji wa sheria iliyoanzisha TMA. Aidha
alisisitiza Bodi kuhakikisha mapato ya Mamlaka yanaongezeka kwa kuhakikisha
ukusanyaji wa Mapato unazingatia vyanzo vyote ambavyo huduma za hali ya hewa
zinatumika kibiashara, sambamba na hayo aliitaka Bodi hiyo pia kuboresha
maslahi ya watumishi ili kuondoa wimbi la watumishi kuhamahama kwa kutafuta
maslahi bora katika taasisi nyingine nje na ndani ya nchi.
Naye
mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dkt. Buruhani Nyenzi alitoa shukrani za dhati kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwateua yeye mwenyewe kuwa Mwenyekiti na Dkt.
Makame Omar Makame kuwa Makamu Mwenyekiti katika kuongoza Mamlaka ya Hali ya
Hewa Tanzania (TMA). Aidha Dkt. Nyenzi alisema anatambua kuwa majukumu
waliyopewa ni mazito na yanahitaji uwajibakaji na kufanya kazi kwa kasi, weledi
na nguvu.
“Nafasi hii ni
nyeti na majukumu tuliyokabidhiwa mimi pamoja na wajumbe wenzangu wa Bodi ni
mazito na yanayohitaji uwajibikaji na kufanya kazi kwa kasi, weledi na nguvu
ili kuweza kuendana na maono makubwa ya Mh. Rais, John Pombe Magufuli”. Alisema
Dkt. Nyenzi.
Kwa upande mwingine wakati akitoa taarifa fupi ya
TMA, Dkt. Agnes Kijazi, alifafanua shughuli zinazofanywa na TMA pamoja na
mafanikio ya Mamlaka ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa
mifumo mbalimbali (software) za kuboresha utendaji kazi wa TMA zilizobuniwa na
wataalam wa ndani ya Mamlaka na hivyo kupunguza gharama kubwa za uendeshaji.
Awali, mmoja wa wajumbe wa Bodi ambaye pia
alimwakilisha Katibu Mkuu (Uchukuzi) Mhandisi. Aron Kisaka alitoa maelezo
mafupi ya utambulisho wa Bodi na kutoa shukrani kwa mhe. Rais pamoja na Mhe. Waziri
kwa uteuzi walioufanya wa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa Bodi.
Uzinduzi wa Bodi mpya umefanyika katika ukumbi wa
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dar es Salaam. Wajumbe wa Bodi hiyo
ni Dkt. Buruhani Nyenzi (Mwenyekiti), Dkt.
Makame Omar Makame (Makamu Mwenyekiti), Kapt. Large Temba (Mjumbe), Bw. Robert
Sunday (Mjumbe), Bi. Marystella Mtalo (Mjumbe), Bi. Jane Kikunya (Mjumbe), Mhandisi.
Aron Kisaka (Mjumbe) na Dkt. Agnes Kijazi (Katibu).