|
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe. Issa Haji Ussi Gavu akipata elimu kutoka kwa mtaalamu wa hali ya hewa ya namna taarifa za hali ya hewa zinavyoweza kusaidia kukuza sekta ya kilimo hapa nchini kupitia maonesho ya siku ya chakula duniani yanayofanyika katika viwanja vya Chamanangwe kisiwani Pemba Tarehe 10 hadi 16 Oktoba 2019. |
|
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe. Issa Haji Ussi Gavu akitoa maelekezo mara baada ya kupata elimu kutoka kwa mtaalamu wa hali ya hewa kupitia maonesho ya siku ya chakula duniani yanayofanyika katika viwanja vya Chamanangwe kisiwani Pemba Tarehe 10 hadi 16 Oktoba 2019. |
|
Waziri
wa nchi Ofisi ya Rais Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe. Issa Haji Ussi
Gavu akipokea zawadi toka kwa meneja wa hali ya hewa kituo cha Pemba Bi.
Bishara Mdowe kupitia maonesho ya siku ya chakula duniani yanayofanyika
katika viwanja vya Chamanangwe kisiwani Pemba Tarehe 10 hadi 16 Oktoba
2019 |
Tarehe 14/10/2019 Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Baraza
la Mapinduzi Zanzibar Mhe. Issa Haji Ussi Gavu aliwataka Mamlaka ya Hali ya
Hewa Tanzania (TMA) kuongeza mbinu za kufikisha taarifa za hali ya hewa kwa
wakulima kwa wakati, alizungumza hayo alipotembelea banda la TMA lililopo kwenye
maonesho ya siku ya chakula duniani yanayofanyika katika viwanja vya
Chamanangwe kisiwani Pemba Tarehe 10 hadi 16 Oktoba 2019.
“Ninawataka muongeze mbinu za kuhakikisha taarifa zenu
zinawafikia wakulima kwa wakati” alisisitiza
Mhe. Issa
Aidha, Mheshimiwa Issa ameipongeza TMA kwa juhudi kubwa
inayoifanya na kufanikiwa kuongeza usahihi wa taarifa za hali ya hewa hapa
nchini. Maonesho
hayo yamefungwa rasmi Tarehe 15 Oktoba 2019 na makamu wa pili wa Rais, baraza
la mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.
No comments:
Post a Comment