Wednesday, October 30, 2019
TMA - JARIDA LA HABARI TOLEO LA 3
Kwa taarifa zaidi tembelea: http://www.meteo.go.tz/uploads/publications/sw1572345256-JARIDA%20LA%20HABARI%20LA%203%20OKTOBA%202019.pdf
Wednesday, October 23, 2019
TMA YAENDELEA KUTOA ELIMU YA SAYANSI YA HALI YA HEWA MASHULENI
Mkurugenzi wa Utafiti na matumizi wa TMA, Dkt. Ladislaus Chang'a akitoa elimu ya sayansi ya hali ya hewa katika shule ya msingi ya Mount Evarest - Dar es salaam. |
Mkurugenzi wa Utafiti na matumizi wa TMA Dkt. Ladislaus Chang'a akitoa elimu ya sayansi ya hali ya hewa katika shule ya msingi ya Mother of Mercy - Dar es salaam. |
Wanafunzi wakipokea zawadi mbalimbali mara baada ya kufanya vizuri katika mitihani ya majaribio waliyopatiwa. |
Wataalam kutoka TMA wakisimika kituo cha kupima mvua (Raingauge) katika shule hizo |
Wednesday, October 16, 2019
MHESHIMIWA ISSA HAJI USSI GAVU AITAKA TMA KUONGEZA MBINU ZA KUFIKISHA TAARIFA ZA HALI YA HEWA KWA WAKULIMA KWA WAKATI.
Tarehe 14/10/2019 Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Baraza
la Mapinduzi Zanzibar Mhe. Issa Haji Ussi Gavu aliwataka Mamlaka ya Hali ya
Hewa Tanzania (TMA) kuongeza mbinu za kufikisha taarifa za hali ya hewa kwa
wakulima kwa wakati, alizungumza hayo alipotembelea banda la TMA lililopo kwenye
maonesho ya siku ya chakula duniani yanayofanyika katika viwanja vya
Chamanangwe kisiwani Pemba Tarehe 10 hadi 16 Oktoba 2019.
“Ninawataka muongeze mbinu za kuhakikisha taarifa zenu
zinawafikia wakulima kwa wakati” alisisitiza
Mhe. Issa
Aidha, Mheshimiwa Issa ameipongeza TMA kwa juhudi kubwa
inayoifanya na kufanikiwa kuongeza usahihi wa taarifa za hali ya hewa hapa
nchini. Maonesho
hayo yamefungwa rasmi Tarehe 15 Oktoba 2019 na makamu wa pili wa Rais, baraza
la mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.
Monday, October 14, 2019
TMA YAHIMIZA WAKAZI WA PEMBA KUTUMIA TAARIFA ZA HALI YA HEWA KATIKA SEKTA YA KILIMO.
Kuanzia tarehe 10 hadi 16 Oktoba 2019 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inashiriki katika maonesho ya siku ya chakula Duniani yanayofanyika katika viwanja vya Chamanangwe kisiwani Pemba, ambapo wataalamu wa hali ya hewa wameendelea kutoa elimu kwa wakazi kisiwani Pemba juu ya umuhimu wa matumizi ya taarifa za hali ya hewa katika sekta ya kilimo.
Meneja wa hali ya hewa kituo cha Pemba Bi. Bishara Mdowe aliongea na wananchi wa Pemba kupitia vyombo vya habari na kuwakumbusha kuwa hivi sasa dunia imekumbwa na mabadiliko ya tabia nchi, hivyo kuwataka kuhacha kufanya shughuli za kilimo kwa mazoea ili kuepusha hasara zisizo za lazima na badala yake waanze kutumia taarifa za hali ya hewa ili kufanya kilimo chenye tija kitakachokuza uchumi wao pamoja na Taifa kwa ujumla.
“Ninawakumbusha wananchi wa pemba, hivi sasa Dunia imekumbwa na mabadiliko ya tabia nchi hivyo tuache kufanya shughuli za kilimo kwa mazoea, ninawahimiza kufuatilia taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na TMA ili kuepusha hasara zisizo za lazima”.
Aidha kwa upande wa wageni waliotembelea katika banda la TMA lililopo katika maonesho hayo akiwemo afisa mdhamini Wizara ya Uchukuzi, Mawasiliano na Usafirishaji Pemba ndugu Hamad Baucha walionesha kufurahishwa na namna elimu inavyotolewa na kuomba elimu iendelee kutolewa mara kwa mara zaidi kupitia vipindi vya redio na runinga. Kauli mbiu ya maonesho hayo ni "Matendo yetu ndiyo Hatma yetu, Lishe Bora kwa Ulimwengu usio na Njaa"
Sunday, October 13, 2019
Friday, October 11, 2019
TMA YATOA MWELEKEO WA HALI YA HEWA KWA MAENEO YANAYOPATA MVUA ZA MSIMU MARA MOJA KWA MWAKA.
Dar es Salaam,Tarehe 10/10/2019: Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa rasmi utabiri
wa msimu wa mvua za mwaka (Novemba 2019 hadi Aprili 2020) na athari zinazoweza
kujitokeza. Utabiri huo ni mahususi kwa maeneo yanayopata mvua mara moja
kwa mwaka ikiwa ni mikoa ya Kigoma, Tabora,Rukwa,Katavi,Mbeya, Songwe,
Njombe,Iringa, Lindi, Dodoma, Singida, Mtwara na Kusini mwa mkoa wa Morogoro.
Akizungumza na waandishi
wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa tatu wa Rais wa WMO Dkt. Agnes
Kijazi aliwataka wananchi wa maeneo hayo kuzitumia vizuri mvua hizo kwa kupata
ushauri kutoka kwa wataalamu wa sekta husika kwa vile maeneo mengi yanatarajiwa
kuwa na mvua za kutosha.
‘Naendelea kutoa rai kwa
wananchi wa mikoa husika kuzitumia mvua hizi kwa kupanda mazao sahihi kwa
kufuata ushauri wa wataalamu, kama tunavyoona maeneo mengi yatarajiwa kuwa na
mvua za juu ya wastani hadi wastani’, alisema Dkt. Kijazi.
Aidha, Dkt. Kijazi
alifafanua kuhusu mvua zinazoendelea kunyesha kwa maeneo ya kaskazini mwa nchi
kwa kusema kuwa mvua hizi ni za msimu wa vuli kwa maeneo yanayopata mvua mbili
kwa mwaka na katika kipindi hiki cha vuli kunatarajiwa kuwa na vipindi vifupi
vya mvua kubwa ambapo alimalizia kwa kuwataka wananchi kuendelea kufuatilia
taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na TMA sambamba na kuchukua tahadhari ya
vipindi vifupi vya mvua kubwa,upepo mkali na mawimbi makubwa, vinavyotarajiwa
kujitokeza katika baadhi ya maeneo.
Utabiri uliotolewa kwa
maeneo yanayopata mvua za msimu mara moja kwa mwaka unaonesha maeneo ya mengi
ya mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora, Mbeya, Songwe, Ruvuma, Njombe, Iringa, Rukwa
Kusini mwa mkoa wa Morogoro, Lindi na Mtwara, yanatarajiwa kupata mvua za juu
ya wastani hadi wastani na maeneo ya mikoa ya Kigoma na Katavi, yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu
ya wastani.
Wednesday, October 9, 2019
WANAHABARI WAKUMBUSHWA UMUHIMU WA KUFIKISHA HABARI ZA HALI MBAYA YA HEWA KWA WAKATI.
Wanahabari katika picha ya pamoja wakati wa warsha ya wanahabari ya kujadili mwelekeo wa msimu wa mvua za mwaka kwa kipindi cha mwezi Novemba 2019 hadi Aprili 2020 na athari zinazoweza kujitokeza. |
Wadau katika picha ya pamoja wakati wa warsha ya wanahabari ya kujadili mwelekeo wa msimu wa mvua za mwaka kwa kipindi cha mwezi Novemba 2019 hadi Aprili 2020 na athari zinazoweza kujitokeza. |
Mmoja wa wadau akichangia mada wakati wa warsha ya wanahabari ya kujadili mwelekeo wa msimu wa mvua za mwaka kwa kipindi cha mwezi Novemba 2019 hadi Aprili 2020 na athari zinazoweza kujitokeza. |
Tarehe
09/10/2019: Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imekutana
na wadau wa sekta mbalimbali na wanahabari ili kujadili mwelekeo wa msimu wa mvua
za mwaka kwa kipindi cha mwezi Novemba 2019 hadi Aprili 2020 na athari
zinazoweza kujitokeza.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo, mgeni
rasmi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa WMO, Dkt.
Agnes Kijazi alisisitiza umuhimu wa vyombo vya habari katika kusambaza taarifa
za hali ya hewa ukiwemo utabiri wa hali ya hewa na tahadhari ya hali mbaya ya
hewa, huku akitolea mfano wa athari zilizoanza kuonekana mwanzoni mwa msimu wa
mvua za vuli za mwaka huu.
“Napenda kusisitiza umuhimu wa warsha hizi ni
kuhakikisha jamii tunayoenda kuihudumia inapata taarifa sahihi, kwa wakati na
kwa lugha inayoeleweka kirahisi, msimu wa vuli umeanza na matukio mengi ya
upepo mkali, mawimbi makubwa na mvua kubwa hivyo taarifa hizi zinakuwa na
manufaa pale ambapo zinatumika kwa wakati’, alisema Dkt. Kijazi. Aidha,
alivishukuru vyombo vya habari nchini kwa kuendelea kusambaza kwa wakati
taarifa za hali ya hewa ikiwa pamoja na tahadhari za hali mbaya ya hewa.
Kwa upande mwingine, Dkt.Kijazi alifafanua kwa
wadau wa sekta mbalimbali sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Na.2 ya 2019.
Alisema lengo la Sheria hiyo ni kuboresha huduma za hali ya hewa hapa nchini na
kutoa mwongozo wa ushiriki wa sekta mbalimbali
katika matumizi ya huduma hizo. Dkt. Kijazi alifafanua vipengele vya
sheria hiyo vinavyowahusu wadau wa huduma za hali ya hewa alipokuwa anafunga
mkutano huo wa wadau.
Aidha, wadau hao walipata fursa ya kutoa ushauri wa
athari zinazoweza kujitokeza kulingana na utabiri wa msimu wa mwaka ulioandaliwa
kwa mikoa inayopata mvua za msimu mara moja kwa mwaka ambayo ni mikoa ya kanda ya magharibi, kati,
nyanda za juu kusini magharibi, kusini mwa nchi, ukanda wa pwani ya kusini
pamoja na maeneo yaliyoko kusini mwa mkoa wa Morogoro.
Kwa upande wa wanahabari waliahidi kuendelea kutoa
taarifa sahihi za hali ya hewa kama zinavyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania na waliishukuru TMA kwa kuendesha warsha hizo ambazo zimeendelea
kuwajengea uwezo wa kuelewa lugha inayotumika katika utabiri wa hali ya hewa.
Warsha hizo
zilifanyika tarehe 08/10/2019 kwa kuwakutanisha wadau wa sekta mbalimbali na
tarehe 09/10/2019 kwa kuwakutanisha wanahabari. Utabiri wa msimu wa mvua za mwaka
kwa kipindi cha mwezi Novemba 2019 hadi Aprili 2020 unatarajiwa kutolewa rasmi kwa
umma kupitia vyombo vya habari siku ya Alhamisi, tarehe 10/10/2019,makao makuu
ya ofisi za TMA, saa tano kamili asubuhi.
TMA YAJIPANGA KUTOA MWELEKEO WA MSIMU WA MVUA ZA MWAKA KWA MWEZI NOVEMBA 2019 HADI APRILI 2020 KWA KUWANOA WANAHABARI
Subscribe to:
Posts (Atom)
Featured Post
DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.
Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...
-
DODOMA; Tarehe 19 Agosti, 2024; Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imekutana na wadau kutoka sekta mbalimbali nchini ili kujipanga na...
-
10 Septemba 2024, Arusha: Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa elimu kwa wadau mbalilmbali wa Ununuzi kuhusu matumizi sahihi ya h...
-
Dar es Salaam, 22 /0 8 /202 4 ; Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa msimu wa mvua za VULI 202 4 kwa maeneo yanayopat...