Tuesday, July 30, 2019
Tuesday, July 23, 2019
TMS YAWA CHACHU KATIKA KUFANIKISHA MALENGO YA TMA KWA KUCHOCHEA MATUMIZI SAHIHI YA TAARIFA ZA HALI YA HEWA KATIKA SEKTA MBALIMBALI HAPA NCHINI.
Matukio mbalimbali kwa picha wakati sekta mbalimbali zikijengewa uwezo juu ya matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa katika hamashauri ya mji Bariadi, Simiyu. |
Matukio mbalimbali kwa picha wakati waandishi wa habari wakijengewa uwezo juu ya matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa katika Halmashauri ya mji Bariadi, Simiyu |
Picha mbalimbali za matukio wakati sekta mbalimbali zikijengewa uwezo juu ya matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa katika mkoa wa Tanga. |
Chama cha
Wataalam wa Hali ya Hewa Tanzania (TMS) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya
Hewa Tanzania (TMA) kimeendelea
kukutana na wadau toka sekta mbalimbali wa kilimo, mifugo, nishati, maafa, maji
pamoja na wanahabari kwa mikoa ya Tanga tarehe 01- 02 Julai2019 na Simiyu
tarehe 08- 09 Julai 2019, katika kuwajengea uwezo wa kutumia taarifa za
hali ya hewa kwa usahihi. Hii ni katika muendelezo wa utekelezaji wa mradi “Weather
and Climate Information Services” (WISER II),
Katika ufunguzi wa
warsha iliyofanyika Simiyu, Rais wa TMS Dkt. Buruhani Nyenzi aliwashukuru wadau
wote kwa ushiriki wao na kuendelea kuwasisitiza kufuatilia na kutumia taarifa
za hali ya hewa katika shughuli zao za kiuchumi.
Aidha Mgeni
rasmi Mhandisi Masha Luhamba ambaye pia
ni Kaimu katibu tawala Mkoa Simiyu alihamasisha
washiriki kuzingatia mafunzo hayo, ambayo
anaamini yatasaidia kufikia malengo ya kimkoa katika kuifanya Simiyu kuwa ya
viwanda katika kuunga mkono juhudi za Rais wa Serikali ya awamu ya tano Mhe.
John Pombe Magufuli yenye lengo la kutufikisha kwenye uchumi wa kati na
viwanda.
“naomba mtambue kuwa mmechaguliwa ninyi kati ya
watendaji wengi wa serikali hapa mkoani Simiyu hivyo nina imani kubwa sana toka kwenu ya kuwa
mabalozi wazuri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania hapa Simiyu kupitia mafunzo
mtakayoyapata na kuhakikisha wananchi wanapata taarifa za hali ya hewa kwa
wakati na kuzielewa ili kusaidia kuongeza tija katika uzalishaji malighafi
ambazo zitatumika katika viwanda na kufanya mkoa wetu uwe wenye viwanda vya
kutosha” alisema Mhandisi Luhamba.
Pia warsha hiyo
ilifanyika katika mkoa wa Tanga, ambapo washiriki waliahidi kuisambaza elimu
hiyo waliyoipata kwa wadau kutoka katika sekta zao hususani wavuvi ili wawe na mazoea ya kufuatilia utabiri wa
hali ya hewa kabla ya kuingia Baharini.
IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Subscribe to:
Posts (Atom)
Featured Post
DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.
Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...
-
10 Septemba 2024, Arusha: Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa elimu kwa wadau mbalilmbali wa Ununuzi kuhusu matumizi sahihi ya h...
-
06 Septemba 2024, Dar es Salaam: Wahandisi nchini wamekumbushwa umuhimu wa huduma za hali ya hewa sambamba na kuchangia gharama za upatik...
-
DODOMA; Tarehe 19 Agosti, 2024; Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imekutana na wadau kutoka sekta mbalimbali nchini ili kujipanga na...