Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya TMA Dkt. Buruhani Nyenzi akizungumza wakati wa kusaini mikataba ya upatikanaji wa Rada mbili za hali ya hewa kwa mikoa ya Mbeya na Kigoma |
Baadhi ya wafanyakazi wa TMA na wanahabari wakishuhudia tukio la kusainiana kwa mikataba ya upatikanaji wa Rada mbili za hali ya hewa kwa mikoa ya Mbeya na Kigoma |
Serikali ya awamu ya tano imejizatiti
katika kuhakikisha huduma za hali ya hewa nchini zinakuwa za viwango vya
kimataifa na za usahihi wa hali ya juu. Katika kufanikisha hili Serikali ya
awamu ya tano iliahidi kuendelea kuongeza mtandao wa Rada za hali ya hewa ili
kufikia Rada saba (7) zinazohitajika kwa nchi nzima.
Serikali kupitia Mamlaka ya Hali ya
Hewa Tanzania, imesaini mkataba wa ununuzi wa Rada mbili za hali ya hewa
zitakazofungwa eneo la Kawetere katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya na eneo la
Nyamoli katika barabara ya kuelekea Bulombora, Kigoma na hivyo kuifanya
Tanzania kuwa na jumla ya mtandao wa rada tano (5). Ikumbukwe kuwa tayari Mamlaka
imeishafunga rada mbili za hali ya hewa huko Kiseke Mwanza na Bangulo Dar es
Salaam pia imeanza utaratibu wa ufungaji wa Rada Mtwara. Hii inaifanya Tanzania
kuwa Taasisi bora kwa uangazi wa wa hali ya hewa kwa njia ya Rada katika ukanda
wa Afrika Mashariki na Kati.
Ununuzi wa Rada hizi mbili (ya nne na ya tano) kwa ajili ya Mbeya na Kigoma umegharimu kiasi cha Tshs. 5,715,971,148.45 (USD 2,497,125) kwa
kila moja na pia utengenezaji na ufungaji wa rada zote mbili utachukua muda wa
miezi kumi na nne hadi kukamilika kwake.
Mtengenezaji wa Rada hizo ni Enterprise
Electronics Corporation (ECC)
Rada
hizi zina uwezo wa kuona hadi kilometa za mkato 450 (Aerial distance) huku
zikizunguka (radius distance) na uwezo halisia wa kuona mpaka matone madogo
sana ya mvua ni kilometa za mkato 250.
Rada za hali ya hewa ni moja ya mitambo inayotumika
kufanya uangazi wa hali ya hewa wa masafa marefu. Mitambo hii husaidia katika
kukusanya data za hali ya hewa zinazoonesha uhalisia wa anga kipindi Radar
inapozunguka. Rada inasaidia;
·
Kujua
kwa wakati maeneo yenye mvua, aina ya mawingu yaliyopo na wakati mwingine hata
kujua ni kiasi gani cha mvua kinachotarajiwa.
·
Kufuatilia
maeneo yenye mvua kubwa na za mawe zinazoambatana na radi na upepo mkali hivyo
kuweza kutoa tahadhari kwa muda muafaka.
·
Kufuatilia
muelekeo wa mifumo inayosababisha hali mbaya ya hewa (mvua za mawe, upepo mkali
na dhoruba).
·
kufuatilia
vimbunga baharini kadri ya upeo wake na hivyo kuweza kutoa tahadhari kutokana
na mwenendo wa vimbunga hivyo.
·
Kufuatilia
upepo unaoweza kuleta madhara kwa usalama wa usafiri wa anga (wind shear) na
·
Kutoa
ushauri kwa watumiaji wa huduma za hali ya hewa ili wachukue tahadhari wakati
wa shughuli zao kiuchumi na kijamii.
·
Kusaidia
kutoa utabiri wa muda mfupi na wakati wa hali mbaya ya hewa.
Wito unatolewa kwa wananchi wote kutoa ushirikiano katika kulinda
na kutunza mitambo hii ya Rada pamoja na vifaa vyote vya hali ya hewa kwa
manufaa ya Taifa letu.
No comments:
Post a Comment