Matukio mbalimbali katika picha wakati wafanyakazi wa TMA wakipata mafunzo ya kutumia mfumo wa serikali wa kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato ya serikali (GePG). |
12/04/2019; DAR ES SALAAM
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
(TMA) imepata mafunzo ya kutumia
mfumo wa serikali wa kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato ya serikali (GePG)
ikiwa niutelezaji wa sheria ya fedha za umma, sura 348 iliyopitishwa na bunge
kifungu cha 44 cha mwaka 2017.
Akizungumza wakati wa kuhitimisha
mafunzo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt.
Agnes Kijazi alieleza kuwa mafunzo hayo ni
mwendelezo wa juhudi za Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) katika kutekeleza
maelekezo yote yanayotolewa na Serikali inayoongozwa na mhe. Rais Dkt. John
Pombe Magufuli kwa lengo la kuongeza tija na ufanisi katika utoaji huduma bora
kwa umma. Alisisitiza kwamba mafunzo
hayo yataiwezesha Mamlaka kuboresha njia za ukusanyaji wa mapato na hivyo kutoa huduma bora kwa
wananchi.
Kwa upande wa washiriki wa mafunzo
hayo, meneja wa fedha na uhasibu Bw. Michael Ntagazwa alieleza faida za mfumo
huo kuwa ni kuboresha utendaji kazi ikiwa pamoja na
urahisi katika kuandaa na kupata taarifa za mapato kwa vituo vyote na kwa
wakati wowote.
Naye mtaalam
kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Jane Kazoba alieleza kuwa mfumo huo
umeunganishwa na ofisi mbalimbali zinazokusanya mapato ya serikali zikiwemo
wizara na taasisi zake na taasis zinazotoa huduma za fedha nchini.
Imetolewa:
Ofisi ya Uhusiano
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
(TMA)
No comments:
Post a Comment