Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) kwa
kushirikiana na Wadau limeandaaa mkutano wa Afrika kuhusu Utoaji wa Huduma za Hali
ya Hewa kwa Usalama wa Usafiri wa Anga (2018 African Conference on Meteorology
for Aviation (ACMA-2018), uliofanyika Saly- Senegal.
Mkutano huo ulifanya majadiliano na kupeana
uzoefu wa huduma za hali ya hewa kwa usafiri wa anga ili kuwa na uelewa wa
pamoja wa fursa na changamoto zilizopo katika Afrika. Aidha, ulilenga kujua
vipaumbele na vihatarishi vya utoaji wa huduma za hali ya hewa kuhusiana na mpango
wa Shirika la Usafiri wa Anga Duniani ICAO Global Air Navigation Plan (GANP)
and aviation System Block Upgrades (ASBU) methodology.
Vile vile, Tanzania ilipata nafasi ya kujadili
kwa pamoja na wanachama wengine athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwa upande
wa usafiri wa anga hususan katika Afrika na kujua mahitaji ya wadau. Aidha,kufanyika
kwa mkutano huo ni utekelezaji wa Azimio la Pili la Mkutano wa Nchi Wanachama
wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani(WMO) kanda ya Afrika (Resolution 2 of the
sixteenth session of WMO Regional Association I - Africa) uliofanyika Praia,
Cabo Verde Februari, 2015.
Makubaliano ya mkutano huo yatawasilishwa kwenye
mkutano wa 17 ujulikanao kama seventeenth session of WMO Regional Association I
unaotarajiwa kufanyika Cairo, Misri mwezi Februari, 2019.
Tanzania iliwakilishwa katika mkutano huo na
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Mwakilishi wa
Kudumu wa Tanzania katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) – Dkt. Agnes
Kijazi pamoja na Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri – Dkt. Hamza Kabelwa na Meneja
wa kitengo cha kusimamia Viwango wa Ubora na Vihatarishi – Dkt Geofrid Chikojo.
Mkutano huo pia ulihudhuriwa na wajumbe wengine wakiwemo kutoka Shirika la
KImataifa la Usafiri wa Usalama wa Anga (ICAO), Shirika la Hali ya Hewa Duniani
(WMO), Taasisi ya Hali ya Hewa Uingereza (UK Met Office), Taasisi ya Hali ya
Hewa Finland (FMI), Wakala wanaosimamia kutoa na Kudhibiti Usafiri wa Anga Nchi
za Mangharibi (ASECNA)
No comments:
Post a Comment