Tanzania kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania inashiriki Mkutano wa 24 wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa (Climate Change
Conference 24) unaoendelea huko Katowice, Poland kuanzia tarehe 3 hadi 14
Desemba 2018.
Mkutano huo umewakutanisha wadau mbalimbali
kutoka duniani kote wakiwemo viongozi wa nchi, mashirika ya kimataifa, taasisi
za kiserikali na zisizo za kiserikali n.k. Ujumbe wa Tanzania umeongozwa na
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Mussa
Sima
Kupitia mkutano huo, Mbunge wa Handeni
Vijijini Mhe. Mboni Mhita na Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi walipata
fursa ya kuongea na Katibu Mkuu wa WMO na kujadili masuala mbali mbali
yanayohusu ushiriki wa Taasisi za Hali ya Hewa za Afrika katika kutekeleza
programu za WMO na misaada WMO inayoweza kutoa kuziwezesha taasisi hizo ikiwa
pamoja na kuongeza wataalam kutoka Afrika katika Secretariat ya WMO.
Aidha mhe. Mboni aliiomba WMO kuendelea kuzisaidia
nchi za Afrika kupata vifaa vya kisasa kulingana na changamoto za mabadiliko ya
hali ya hewa ili kufanikisha utoaji wa taarifa sahihi za hali ya hewa kwa
maendeleo endelevu.
Aliongezea kwa kutoa mfano wa umuhimu wa
taarifa za hali ya hewa kwa jimbo lake, ambapo alielezea namna walivyo nufaika
na kilimo cha mhogo (mazao yanayostahimili ukame) baada ya kupata utabiri wa
msimu mvua kutoka TMA.
Kwa upande wa Dkt. Kijazi aliwashukuru WMO
kwa ushirikiano wanaoendelea kuutoa kwa TMA ikiwemo kufadhili baadhi ya miradi
ya huduma za hali ya hewa nchini.
No comments:
Post a Comment