Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imeendelea kutoa mafunzo ya
hali ya hewa kwa wanahabari ili kuwajengea uwezo wanahabari kuelimisha jamii
juu ya umuhimu na matumizi sahihi ya huduma za hali ya hewa. Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dkt. Agnes Kijazi amefungua rasmi mafunzo ya
wiki tatu ya hali ya hewa kwa ajili ya watangazaji na watayarishaji vipindi vya
Azam Media. Mafunzo hayo yanatolewa na Mamalaka ya Hali ya Hewa Tanzania na
Shirika la Hali ya Hewa Duniani WMO
Mafunzo hayo yanatarajiwa kuwawezesha watangazaji na
watayarishaji wa vipindi kuwa na uelewa wa masuala ya hali ya hewa ili kufikisha
taarifa hizo katika lugha rahisi lakini inayowakilisha taarifa hizo kadri
ilivyokusudiwa. Mafunzo hayo ya wiki tatu yanatarajiwa kumalizika tarehe 20 mwezi Mei
mwaka huu.
No comments:
Post a Comment