Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Dkt. Ladislaus Chang'a akifungua warsha ya wadau inayohusu kuimarisha usambazaji na matumizi ya taarifa na huduma zitolewazo na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
Mkurugenzi wa Huduma Saidizi Bw. Laurent Shauri akimkaribisha mgeni rasmi kufungua warsha ya wadau
inayohusu kuimarisha usambazaji na matumizi ya taarifa na huduma
zitolewazo na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
Maafisa kilimo kutoka Wilaya ya Kiteto na Longido wakielezea namna walivyonufaika na elimu kutoka TMA katika warsha ya wadau
inayohusu kuimarisha usambazaji na matumizi ya taarifa na huduma
zitolewazo na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
Meza kuu pamoja na wadau mbalimbali wakiendelea kupata uzoefu katika warsha ya wadau
inayohusu kuimarisha usambazaji na matumizi ya taarifa na huduma
zitolewazo na Mamlaka ya Hali ya Hewa TanzaniaNa: Monica Mutoni
Mamlaka
ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na Wilaya za
Longido na Kiteto katika kuhakikisha matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa
yanafanyika sambamba na jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. TMA
imetumia uzoefu wa Kiteto na Longido ili kuimarisha huduma katika maeneo
mengine ya nchi yetu, wakati ilipoandaa warsha iliyowakusanisha wadau
mbalimbali wa sekta ya kilimo na mifugo. Warsha hiyo ilifanyika tarehe 04 Mei
2016, Blue Pearl, Dar es Salaam.
Juhudi
hizi zinafanyika kwa kushirikiana na mpango malumu wa kidunia (Global
Frameworks for Climate Services (GFCS)) wa kuimarisha utoaji na usambazaji wa taarifa za hali
ya hewa
ili kuongeza tija na ufanisi katika shughuli za uzalishaji na maendeleo
na pia kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Mpango huu umefadhiliwa na
Serikali ya Norway.
Utekelezaji wa mpango wa GFCS umelenga Wilaya
za Kiteto na Longido ambazo ni mojawapo ya maeneo yaliyoathirika na mabadiliko
ya hali ya hewa na ikaonekana ni muhimu mradi huu ufike maeneo ambayo yana
mahitaji ya taarifa za hali ya hewa hasa kwa wakulima na wafugaji wanaoishi
pembezoni mwa Tanzania.
Mabadiliko
ya hali ya hewa yamejidhihirisha sana hasa katika kubadilika kwa mtawanyiko wa
mvua, misimu ya mvua kuwa mifupi, kupungua kwa wingi wa mvua na kuongezeka kwa
joto.
No comments:
Post a Comment