Meneja Kitengo cha Utabiri Bw. Samuel Mbuya (aliyesimama) akitoa ufafanuzi nwa kina kuhusiana na EL NINO kwa wanahabari
Wanahabari wakiwa kazini tayari kwa kueleimisha umma kuhusiana na utabiri uliotolewa na TMA.
Kutokana na mwelekeo wa mifumo ya hali ya hewa iliyopo
na inayotarajiwa, mvua za vuli zinatarajiwa kuwa kama ifuatavyo:
(i)
Mvua za vuli
(kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua)
Msimu wa mvua wa miezi ya Oktoba hadi Disemba (vuli) ni mahususi katika maeneo ya
nyanda za juu kaskazini mashariki (Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara),
pwani ya kaskazini (Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Morogoro-kaskazini
pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba), kanda
ya Ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, Geita, Simiyu na Shinyanga) na
kaskazini mwa mkoa wa Kigoma. Mvua zinatarajiwa kuwa za juu ya wastani hadi
wastani kwa maeneo mengi. Mvua hizo zinatarajiwa kuanza mapema katika wiki
mbili za mwisho za mwezi Septemba 2015 katika kanda ya ziwa Victoria na katika maeneo
machache ya Pwani ya kaskazini.
Kanda ya Ziwa Victoria:
(Mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, Geita, Simiyu na Shinyanga): Mvua zinatarajiwa kuanza kati ya wiki ya tatu ya mwezi Septemba 2015 katika mikoa ya Kagera na Mara
na kusambaa katika Mikoa mingine. Mvua zinatarajiwa kuwa za juu ya wastani hadi
wastani katika maeneo hayo.
Ukanda wa Pwani ya Kaskazini:
(Maeneo ya kaskazini mwa mkoa wa Morogoro,
mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani pamoja na Visiwa vya Unguja na
Pemba):
Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi Septemba, 2015 na
zinatarajiwa kuwa za juu ya wastani hadi
wastani katika mikoa ya Tanga, pamoja na
visiwa vya Unguja na Pemba; na wastani hadi juu ya wastani katika maeneo wa mikoa
ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro.
Nyanda za juu Kaskazini
Mashariki: (Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara):
Mvua katika maeneo haya zinatarajiwa kuanza katika
wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba , 2015
katika Mkoa wa Arusha na kusambaa katika mikoa mingine na zinatarajiwa kuwa za juu
ya wastani hadi wastani kwa ujumla.
(ii) Mvua za Msimu (Novemba – Aprili) kwa maeneo yanayopata msimu
mmoja wa mvua.
Msimu wa mvua za Novemba hadi Aprili ni mahususi kwa
maeneo ya Magharibi mwa nchi(Mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi na Rukwa),
kanda ya kati (Mikoa ya Singida na Dodoma), nyanda za juu kusini-Magharibi (Mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe na kusini
mwa Morogoro), kusini mwa nchi na pwani ya kusini (mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara) zinatarajiwa kuanza mwezi
Novemba 2015. Mvua katika maeneo mengi
zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani. Hata hivyo, maeneo machache ya
mikoa iliyo kusini zaidi mwa nchi yanatarajiwa kupata mvua za chini wastani
kama ifuatavyo;
Kanda ya Magharibi (Mikoa ya
Kigoma, Tabora, Katavi na Rukwa):
Mvua za msimu zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya
wastani katika mikoa ya Tabora, Kigoma, Rukwa na Katavi. Kaskazini mwa mikoa ya
Tabora na Kigoma (Wilaya ya Kibondo) kunatarajiwa kuwa na mvua za juu ya wastani
hadi za wastani. Mvua katika maeneo haya zinatarajiwa kuanza katika wiki ya kwanza
ya mwezi Novemba, 2015.
Kanda ya kati (Mikoa ya
Singida na Dodoma):
Mvua za msimu zinatarajiwa kuanza wiki ya pili na tatu
ya mwezi Novemba na zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika
maeneo mengi ya mikoa ya Singida na Dodoma. Hata hivyo maeneo ya kaskazini mwa
mikoa ya Dodoma na Singida yanatarajiwa kuwa na mvua za juu ya wastani hadi
wastani.
Nyanda za juu Kusini
Magharibi: (Mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe na kusini mwa Morogoro):
Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi Novemba na
zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi. Hata
hivyo kusini mwa mkoa wa Njombe na baadhi ya maeneo ya kusini mwa mkoa wa
Morogoro (Mahenge) mvua za wastani hadi chini ya wastani zinatarajiwa.
Maeneo ya kusini na pwani ya
kusini (Mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara)
Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi Novemba
2015 na zinatarajiwa kuwa za wastani hadi chini ya wastani katika maeneo mengi.
Hata hivyo maeneo machache ya upande wa
mashariki mwa mikoa ya Lindi na Mtwara yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani.
Izingatiwe
kuwa pamoja na kuwapo kwa uwezekano wa matukio ya mvua kubwa katika maeneo
yanayotarajiwa kupata mvua juu ya wastani, hali hiyo pia inaweza kujitokeza
katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani.
Matukio ya Vimbunga katika
eneo la kusini magharibi mwa bahari ya Hindi yanatarajiwa kuchangia katika
mwenendo wa mvua hapa nchini.
No comments:
Post a Comment