Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania (TMA) Dkt. Agnes Kijazi amekutana na baadhi ya wanahabari kutoka
vyombo mbali mbali vya habari nchini katika warsha ya siku moja iliyofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ubungo Plaza Dar es Salaam tarehe 01 Septemba
2015.
Katika warsha hiyo Dkt. Kijazi aliwaasa wanahabari
kuhusiana na lugha inayotumika sambamba na elimu ya kina kuhusiana na EL-NINO.
‘Tunatambua mchango mkubwa wa vyombo vya habari nchini hivyo Mamlaka imeandaa
warsha hii tukiwa na nia ya kupata na kutoa mrejesho wa lugha gani itumike ili
kuwarahisishia wanahabari na jamii kwa ujumla kuelewa taarifa za hali ya hewa
hususani suala la El Nino’ alisema Dkt. Kijazi
Aidha mtaalamu Bw. Samuel Mbuya Kutoka TMA
alifananua kuhusiana na namna El Nino inavyotokea na sababu zake kwa
kuzungumzia ongezeko la joto katika Bahari ya Pasifiki hivyo kuchangia
kubadilisha mifumo ya hali ya hewa kwa dunia nzima.
Kwa upande wa wanahabari, Bi. Grace Kingalame kutoka TBC1 alisema ‘Semina
ni hii inatusaidia wanahabari kujifunza vitu vingi kuhusiana na hali ya hewa
jambo ambalo linatupa uwanja mpana wa kuandika habari zinazohusu masuala ya
hali ya hewa kwa usahihi zaidi na hata kuwafikia wananchi tukiwa na taarifa
zilizo sahihi kama vile tahadhari za majanga yanayosababishwa na mvua au
mabadiliko ya tabia nchi. Hivyo ni vyema Mamlaka ikaendelea kutoa mafunzo haya
mara kwa mara kwa ili kuweka mazingira mazuri ya taarifa zake kuripotiwa kwa usahihi’Alisema
Grace.
TMA imekuwa ikiandaa warsha mbalimbali kwa wadau
mbalimbali wakiwemo wanahabari katika mwendelezo wa utoaji elimu ya sayansi ya
hali ya hewa pamoja na kudumisha ushirikiano baina ya Mamlaka na watumiaji wa
taarifa za hali ya hewa ambao ni wadau kutoka sekta mbalimbali.
Akifungua warsha hiyo Dkt. Kijazi alisema Mamlaka
itatoa mwelekeo wa mvua za Vuli kesho tarehe 2 Septemba 2015 saa tano asubuhi.
Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dk.Kijazi akisalimiana na wanahabari katika warsha iliyofanyika
Wanahabari wakiendelea na warsha katika ukumbi wa mikutano wa TMA-Makao Makuu tarehe 01 Septemba 2015
IMETOLEWA NA MONICA MUTONI;
AFISA UHUSIANO, MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.
No comments:
Post a Comment