Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),Dkt.Agnes Kijazi amefungua rasmi
mafunzo ya utunzaji wa mazingira na ulinzi kwa nchi za Kusini mwa Afrika.
Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Dkt. Kijazi, Kaimu Mkutugenzi Mkuu Dkt.
Pascal Waniha alielezea kwa kina uhusiano uliopo kati ya hali ya hewa na
mazingira, hivyo utunzaji wa mazingira ni chachu katika maendeleo endelevu ya
nchi zetu. ‘Ni matarajio yangu kuwa mafunzo haya yataongeza uelewa mkubwa kati
ya hali ya hewa na mazingira yetu hivyo kuchangia katika kuimarisha uhusuiano
wake kwa maendeleo endelevu ya nchi zetu,.Alisema Dkt.Kijazi.
Aidha aliwashukuru wadhamini wa mradi na mafunzo kwa
kuendelea kuchangia katika uborshaji wa huduma za hali ya hewa nchini za Kusini
mwa Afrika hususan Tanzania. ‘Umoja wa
Ulaya kupitia Umoja wa Afrika na Umoja wa Nchi za Kusini mwa Afrika wameendelea kuisaidia Tanzania kwa njia
mbalimbali kama vile taarifa za ukame
(TMA), madhara ya moto (Wizara ya Utalii), taarifa za kilimo (Wizara ya
Kilimo), Mafuriko (Kitengo cha Maafa) na usalama wa bahari ya Hindi
(TAFIRI) vilevile usimikaji wa vifaa na uwezekano wa TMA
kutumia satelaiti za Ulaya katika uchambuzi wa taarifa za hali ya hewa. Kwa
kupitia hayo yote Tanzania imezidi
kuboresha usahihi wa huduma zake hivyo
kusaidia kupunguza athari kwa mazingira yetu sambamba na kujiandaa kukabiliana
na athari hizo’.Aliongezea Dkt. Kijazi.
Tanzania imeandaa
mafunzo hayo ya siku tano yaliyofanyika
tarehe 7 hadi 11 Septemba 2015 kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali kutoka
Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Kilimo na Usalama wa Chakula,TMA,
Taasisi ya Misitu,TAFIRI, Kitengo cha Maafa, Chuo cha Ardhi na wadau
mbalimbali. Mafunzo hayo yanaendeshwa na wataalam kutoka Tanzania, Chuo Kikuu
cha Zimbabwe, Namibia na Botswana. Lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha taarifa
zinazotolewa ziko sahihi kwa utoaji maamuzi ya
maendeleo ya Taifa letu.
No comments:
Post a Comment