Taarifa hii inatoa mwelekeo wa mifumo
ya hali ya hewa, joto na mvua katika kipindi cha miezi ya Juni hadi Agosti
(JJA) 2014.
1. MIFUMO YA HALI YA HEWA
Mifumo ya hali ya hewa inaonesha uwezekano wa
kuongezeka kwa joto la bahari katika eneo la ukanda wa Tropiki la bahari ya
Pasfiki kwa kipindi cha miezi ya Juni hadi Agosti 2014. Ongezeko kidogo la joto
linatarajiwa katika ukanda wa magharibi ya bahari ya Hindi. Aidha joto katika
bahari ya Atlantik linatarajiwa kuwa chini ya wastani. Hali hiyo inatarajiwa
kusababisha upepo kuvuma kutoka magharibi ukielekea mashariki katika maeneo
mengi ya nchi. Joto la bahari la juu ya wastani linatarajiwa katika eneo la
ncha ya kusini ya bara la Afrika hivyo kuathiri msukumo wa upepo wa kusi katika
kipindi cha miezi ya Juni hadi
Agosti2014. Hali hii inatarajiwa
kusababisha hali ya baridi katika kipindi hicho. Aidha, vipindi vifupi vya mvua
za vinatarajiwa katika maeneo machache ya ukanda wa Ziwa Viktoria, ukanda wa
pwani na katika maeneo ya miinuko.
2:
VIWANGO VYA CHINI VYA JOTO NA MVUA: JUNI HADI AGOSTI, 2014
2.1
MATARAJIO YA VIWANGO VYA CHINI VYA JOTO KWA MIEZI YA JUNI HADI AGOSTI 2014
Kindi cha mwezi Juni hadi Agosti, maeneo mengi ya nchi yanarajiwa kuwa
makavu na yenye hali ya baridi katika majira haya ya kipupwe. Mifumo ya hali ya hewa inaonesha kuwa na hali ya joto la
wastani katika kipindi cha miezi ya Juni hadi Agosti 2014 katika maeneo mengi.
Aidha, izigatiwe kuwa hali ya baridi inatarajiwa zaidi nyakati za usiku hadi
mapema asubuhi. Matarajio ya viwango vya chini vya joto katika kipindi hicho ni
kama ifuatavyo:
Ukanda wa ziwa Victoria (Mikoa ya Mwanza,
Mara, Chato, Kagera, Shinyanga na Simiyu)
Hali ya joto inatarajiwa kuwa juu ya wastani(Juu ya nyuzi joto 17.2 0C) katika maeneo mengi. Hata hivyo,
katika maeneo ya kusini ya mikoa ya Shinyanga na Simiyu hali ya joto inatarjiwa
kuwa chini ya wastani.
Ukanda wa pwani ya kaskazini (Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani, maeneo
ya kaskazini ya mkoa wa Morogoro pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba)
Hali ya joto inatarajiwa kuwa juu ya wastani(Juu ya nyuzi joto 22.9 0C) katika maeneo mengi. Hata hivyo, katika maeneo ya miinuko ya mkoa wa Tanga
hali ya joto inatarajiwa kuwa chini ya wastani(Chini ya nyuzi joto 15.9 0C).
Ukanda wa nyanda za juu kaskazini mashariki (Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha
na Manyara)
Hali ya joto inatarajiwa kuwa ya wastani(Kati ya nyuzi joto 13.0 0C na 15.8 0C) katika maeneo
mengi. Hata hivyo, katika maeneo ya miinuko viwango vya joto vinatarajiwa kuwa
chini ya wastani(Chini ya nyuzi joto 13.0
0C).
Ukanda wa magharibi (Mikoa ya Kigoma, Tabora na Katavi)
Hali ya joto inatarajiwa kuwa ya wastani(Kati ya nyuzi joto 14.9 0C na17.0 0C) katika maeneo mengi. Hata hivyo, katika maeneo ya
kaskazini ya mkoa wa Kigoma (Kibondo) hali ya joto inatarajiwa kuwa ya wastani(Juu ya nyuzi joto 17.0 0C).
Ukanda wa kati (Mikoa ya Singida na Dodoma)
Hali ya joto inatarajiwa kuwa ya
wastani(Kati ya nyuzi joto14.1 0C
na 14.7 0C ) katika maeneo mengi. Hata
hivyo, vipindi vya upepo mkali wenye kuambatana na baridi vinatajiwa katika
maeneo hayo.
Ukanda wa pwani ya kusini (Mikoa ya
Mtwara na Lindi)
Hali ya joto inatarajiwa kuwa juu ya
wastani(Juu ya nyuzi joto 19.10C)
katika
maeneo mengi.
Ukanda wa kusini
(Mkoa wa Ruvuma)
Hali ya joto inatarajiwa kuwa chini ya
wastani(Chini ya nyuzi joto 11.80C) hususan maeneo ya magharibi mwa mkoa wa Ruvuma(Songea na mwambao wa Ziwa
Nyasa). (Aidha, viwango vya joto la wastani vinatarajiwa kwa maeneo mengine ya
ukanda wa kusini.)
Ukanda wa nyanda za juu kusini-magharibi (Mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe
pamoja na maeneo ya kusini ya mkoa wa Morogoro)
Hali ya joto inatarajiwa kuwa ya baridi kali ambapo viwango vya joto
vinatarajiwa kuwa chini ya wastani(Chini ya nyuzi joto 6.00C). Hata hivyo, katika maeneo ya kaskazini ya mkoa wa
Iringa hali ya joto inatarajiwa kuwa ya wastani.
2.2 MWELEKEO WA MVUA
KWA KIPINDI CHA JUNI HADI AGOSTI 2014
Kipindi cha mwezi Juni hadi Agosti kwa kawaida
huwa ni kikavu kwa ujumla, hata hivyo vipindi vifupi vya mvua vinatarajiwa
katika maeneo ya ukanda wa ziwa Victoria, nyanda za juu kaskazini mashariki na
pwani ya kaskazini . Hivyo matarajio yake ni kama ifuatavyo:
Ukanda wa ziwa Victoria (Mikoa ya
Mara na Kagera)
Vipindi vya mvua ya wastani vinatajiwa katika
maeneo hayo, hususan miezi ya Julai na Agosti 2014
Ukanda wa pwani ya kaskazini (Mikoa
ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani, maeneo ya kaskazini ya mkoa wa Morogoro pamoja
na visiwa vya Unguja na Pemba)
Vipindi vya mvua za wastani vinatajiwa katika
maeneo haya, hususan mwishoni mwa mwezi Juni na katika kipindi cha miezi ya Julai na Agosti 2014
Ukanda wa nyanda za juu
kaskazini-mashariki (Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara)
Vipindi vya mvua za wastani vinatajiwa katika
maeneo hayo, hususan maeo yenye miinuko na katika miezi ya Julai na Agosti
2014.
3: ATHARI NA USHAURI
Katika kipindi hicho
hali ya hewa inatarajiwa kuwa ya wastani katika maeneo mengi na vipindi vya
baridi kali katika baadhi ya maeneo. Hivyo, kwa shughuli zinazotegemea hali ya
joto wadau wanashauriwa kuchukua hatua stahiki ili kukabiliana na madhara
yanayo weza kutokea kutokana hali ya hewa inayotarajiwa. Pamoja na utabiri huu
wa muda mrefu, ni muhimu pia watumiaji wakazingatia taarifa za hali ya hewa
zinazotolewa kwa vipindi vifupi.
Mamlaka inawashauri watumiaji wa taarifa za hali ya hewa waendelee
kutafuta, kupata na kufuata ushauri wa
wataalamu katika sekta husika.
Mamlaka
ya Hali ya Hewa Tanzania itaendelea kufuatilia mifumo ya hali ya hewa na kutoa
mrejeo kila inapobidi.
No comments:
Post a Comment