Rais
wa Shirikia la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Prof. David Grimes ( wanne kushoto kutoka mstari wa mbele) na
Katibu Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Michel Jarraud (watatu kutoka
kushoto mstari wa mbele) katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati Kuu ya
Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO EC). Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya
Hewa, Dkt Agnes Kijazi (wa kwanza kutoka kushoto waliosimama) akiwa miongoni
mwa wajumbe 37 wa kamati hiyo kuu ya WMO.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dkt. Agnes Kijazi akiwa mmoja wa wajumbe
wa kamati kuu ya Shirika la Hali ya Hewa
Duniani anashiriki mkutano wa 66 wa Kamati Kuu ulioanza tarehe 18 Juni 2014
huko Geneva. Mkutano wa mwaka huu utajadili masuala ya hali ya hewa katika
maeneo yafuatayo : Upunguzaji wa madhara yatokanayo na hali mbaya ya hewa,
Utoaji huduma za hali ya hewa, mpango maalum wa kuhakikisha huduma za hali ya
hewa zinawafikia walengwa zikiwa na ubora (Global Framework for Climate
Services-GFCS), Mkakati endelevu wa
kujenga uwezo, mfumo wa uangazi wa hali ya hewa wa Shirika la Hali ya Hewa
Dunia na shughuli za utafiti. Kwa maelezo zaidi tembelea www.wmo.int
IMETOLEWA NA: MONICA MUTONI , AFISA UHUSIANO,TMA
No comments:
Post a Comment