Saturday, June 21, 2014
KATIBU MKUU WA SHIRIKA LA USAFIRI WA ANGA DUNIANI (ICAO) ATEMBELEA OFISI ZA HUDUMA ZA HALI YA HEWA KWA USAFIRI WA ANGA NCHINI (TMA)
Katibu Mkuu wa ICAO Bw. Raymond Benjamin akipata maelezo mafupi kutoka kwa Kaimu Meneja Huduma za Hali ya Hewa kwa Usafiri wa Anga Bw. John Mayunga alipotembelea Kituo cha Hali ya Hewa kilichopo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Katika ziara hiyo Bw Raymond alipendezewa na jinsi Mamlaka ilivyoboresha huduma kwa kutumia teknolojia ambapo wateja wanapata ‘flight Folders’ za taarifa za hali ya hewa kwa njia ya kielekronikali (Aviation Information System (AIS). Huduma hii ni moja ya maboresho yaliyofanywa na TMA katika kukidhi matakwa ya wateja wa usafiri wa anga kwa kuzingatia sera ya ubora (QMS) ya Mamlaka yenye kusisitiza uboreshaji wa huduma kulingana na mahitaji ya wakati husika. TMA ni moja ya taasisi za hali ya hewa chache na za awali kutunikiwa cheti cha ubora wa Kimataifa (ISO:9001:2008) katika ukanda wa nchi za Afrika na kuendelea kukidhi matakwa ya kukimiliki cheti hicho mpaka sasa
Featured Post
DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.
Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...
-
10 Septemba 2024, Arusha: Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa elimu kwa wadau mbalilmbali wa Ununuzi kuhusu matumizi sahihi ya h...
-
06 Septemba 2024, Dar es Salaam: Wahandisi nchini wamekumbushwa umuhimu wa huduma za hali ya hewa sambamba na kuchangia gharama za upatik...
-
Morogoro, Tanzania; 16 Oktoba 2024. Kamati Tendaji ya Utekelezaji wa Mradi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Kuimarisha Uangazi wa Hali ya H...