Monday, June 2, 2025

TMA YAPONGEZWA KWA KUIMARISHA USHIRIKISHWAJI WA WADAU KATIKA KUONGEZA UELEWA WA MATUMIZI SAHIHI YA TAARIFA ZA HALI YA HEWA NA SHERIA YA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.












Dodoma; Tarehe 30 Mei, 2025;

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imepongezwa na kuhimizwa kuendeleza ushirikiano na wadau wa sektambalimbali za kiuchumi na Kijamii ili kuongeza uelewa wamatumizi sahihi ya huduma za hali ya hewa pamoja na ufanisikatika  uzingatiaji wa sheria Namba 2 ya mwaka 2019 ya mamlaka ya hali ya hewa Tanzania.

 

Hayo yalisemwa na mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Hali yahewa Tanzania(NMTC) Dkt, Emmanuel Mpeta KatikaUfunguzi wa warsha ya uelewa wa huduma  za hali ya hewa, zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kwawadau kuitoka sekta mbalimbali nchini, wakiwemoWanahabari. Mafunzo haya yalifanyika kuanzia Tarehe 27 – 30, Mei 2025  kwenye ukumbi wa Royal village jijiniDodoma.

 

“Nawapongeza TMA kwa kuendelea kuwashirikisha wadauwa sekta mbalimbali  kw lengo la kuimarisha matumizi yataarifa ya za hali ya hewa katika shughuli za kijamii nakiuchumi. Warsha hii ni fursa muhimu ya kuboresha hudumaza hali ya hewa na kuimarisha matumizi sahihi ya huduma zahali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya HewaTanzania, ikiwemo uzingatiaji wa Sheria ya Mamlaka ya Haliya Hewa Na.2 ya 2019 katika shughuli zinazotumia au zinazotakiwa kutumia huduma za hali ya hewa nchini. Warshahii pia ni fursa ya kujenga na kuimarisha uelewa kuhusiana nachangamoto na fursa za mabadiliko ya hali ya hewa na Tabianchi.” alisema Dkt. Mpeta

 

Dkt Mpeta alisisitiza pia umuhimu wa wadau wote kuzingatiasheria Na 2 ya Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania katikashughuli zao za kila siku za kiuchumi na kijamii. “Utekelezajiwa sheria ya Mamlaka unaambatana na jukumu la kusimamiahuduma za hali ya hewa pamoja na udhibiti  wa shughuli zahali ya hewa hapa nchini. Mkutano huu ni muhimu katikakuwajengea wadau uelewa wa nini wanapaswa kufanya kwamujibu wa Sheria”.

 

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Mabadiliko yaTabianchi Dkt, Ladislaus Chang’a aliwashukuru wafadhili waMradi wa  “WISER” na washirika wengine kwa kuendeleakushirikiana na TMA katika kuimarisha huduma za hali yahewa.

Aidha, Dkt. Chang’a alisisitiza umuhimu wa  kuzingatiamatumizi sahihi ya huduma za hali ya hewa katika kufanyamaamuzi stahiki wakati wote. Vilevile aliendelea kuvishukuruvyombo vya habari kwa kuendelea kuwa kiungo cha kutoahabari sahihi za hali ya hewa kwa jamii.

 

Warsha hii imehusisha wadau kutoka sekta mbalimbali zakiuchumi na kijamii nchini kama vile nishati, kilimo, maji, habari, maafa, Serikali za Mitaa pamoja na Sekta binafsi. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inaendelea na  juhudi zakuhakikisha jamii inapata uelewa mpana wa taarifa za hali yahewa kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa matumizi ya taarifa hizi kwenye shughuli za kiuchumi na kijamii.

Saturday, May 24, 2025

SULUHU MGAWANYO WA MAPATO WA HUDUMA ZA USAFIRI WA ANGA NCHINI YAPATIKANA.

 









Dar es Salaam; Tarehe 23 Mei 2025;

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) pamoja na Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) wafanikisha upatikanaji wa suluhu ya mgawanyo wa mapato yatokanayo na huduma za usafiri wa anga nchini.

Suluhu hiyo imepatikana kupitia kusainiwa kwa mkataba wa makubaliano ya pamoja baina ya wakuu wa taasis hizo katika ukumbi wa mikutano wa TAA uliopo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, tarehe 23 Mei 2025.

Mkataba huo unafuatia kuundwa kwa mfumo wa kielektroniki (Ankara Jumuishi) utakaosaidia kuimarisha uwazi, ufanisi na tija katika mgawanyo wa mapato yatakayokuwa yamekusanywa kwa kuingizwa moja kwa moja kwenye taasis husika kulingana na asilimia zilizokubalika. Mfumo unatarajiwa kuanza kutumika kuanzia tarehe 1 Julai 2025.

Wakizungumza katika zoezi la utiaji saini, Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Abdul Mombokaleo alieleza kuwa mfumo huo wa kielektroniki utarahisisha mgawanyo wa mapato na kuwezesha kila taasis kupata mgao wake kwa wakati ili kusukuma gurudumu la maendeleo ya nchi yetu. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC), Dkt. Ladislaus Chang’a aliwashukuru viongozi wenzake kwa kufanikisha kukamilika kwa mfumo huo na kusisitiza kuwa mfumo huo utachangia sana kuongeza tija na ufanisi katika utendaji kwa kupunguza muda na nguvu kubwa iliyokuwa inatumika kufuatilia mapato yatokanayo na huduma zitolewazo na kila taasis

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Mhandisi Peter Ulanga alipongeza muitikio kutoka pande zote wa kutekeleza maelekezo ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufanya mifumo ya taasis za serikali kusomana, naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Bw. Daniel Malanga alipongeza hatua iliyofikiwa sababu itaboresha utoaji huduma ndani ya viwanja vya ndege nchini.




TMA NA CRDB ZAWANOA MAAFISA UGANI MBEYA, NJOMBE, IRINGA NA SONGWE








Wataalamu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) kwa kushirikiana na Benki ya CRDB kupitia mradi wa Tanzania Agriculture Climate Adaptation Technology Deployment Project (TACATDP) wamewajengea uwezo Maafisa Ugani wa namna bora ya kutafsiri na kutumia taarifa za hali ya hewa hususani katika shughuli za kilimo.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi (TMA) Bw. Elias Elipiki, alisema mafunzo hayo yanawalenga Maafisa Ugani kwani wao ni daraja kati ya TMA na wakulima, hivyo mafunzo haya yanalenga kutoa elimu  ya namna sahihi ya kutafsiri taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka na kuwawezesha wakulima kufanya mipango sahihi juu ya shughuli za kilimo kwa msimu husika.

Aidha, Meneja Uhusiano kutoka CRDB ambaye pia ni msimamizi wa utoaji wa mikopo inayozingatiwa uhifadhi wa mazingira katika mradi wa (TACATDP) Bw. Karim Kindole,  alisema CRDB na TMA wana ushirikiano katika kuwajengea uwezo Maafisa Ugani namna ya kudhibiti na kuwasaidia wakulima kupata taarifa sahihi za mabadiliko ya hali ya hewa.

Naye, Afisa Kilimo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Bw. Sostenesi Silayo, aliwashukuru TMA na CRDB kwa kuwapa nafasi Maafisa Ugani kupata elimu ambayo wataitumia katika kuwashauri wakulima kulima kilimo sahihi kutokana na hali ya hewa husika na kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao mengi.

Thursday, May 22, 2025

TMA YATOA RASMI UTABIRI WA MSIMU WA KIPUPWE 2025.

 




Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa rasmi mwelekeo wa hali ya hewa kwa msimu wa Kipupwe unaoanzia Mwezi Juni hadi Agosti (JJA) 2025. Katika taarifa hiyo imeelezea mwelekeo wa hali ya joto na upepo unatarajiwa kujitokeza na kutoa ushauri kwa sekta mbalimbali juu ya hatua za kuchukua katika kukabiliana na matarajio hayo.

 

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC), Dkt. Ladislaus Chang’a alieleza kuwa vipindi vya baridi kali vinatarajiwa kujitokeza mwezi Julai katika baadhi ya maeneo na hali ya baridi ya wastani hadi joto kiasi inatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi, aliendelea kusema kuwa upepo wa wastani unatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi huku vipindi vifupi vya upepo mkali vikitarajiwa katika maeneo ya ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi kwa kipindi cha miezi ya Juni na Julai 2025.

 

‘Hali ya baridi ya wastani hadi joto kiasi inatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi. Hata hivyo, hali ya baridi ya wastani hadi baridi kali inatarajiwa katika maeneo ya mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Rukwa, Singida pamoja na maeneo ya magharibi mwa mkoa wa Dodoma. Vipindi vya baridi zaidi vinatarajiwa kujitokeza katika mwezi Julai huku vipindi vya mvua za nje ya msimu vikitarajiwa katika maeneo ya ukanda wa Ziwa Victoria, ukanda wa mwambao wa pwani pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.’ Alizungumza Dkt. Chang’a

 

’Aidha, napenda kuwajulisha kuwa Msimu wa Kipupwe 2025 unatarajiwa kutawaliwa na upepo wa wastani utakaovuma kutoka Kusini Mashariki kwa maeneo mengi ya nchi, na vipindi vichache vya upepo mkali utakaovuma kutoka kusini (upepo wa kusi) hususan katika kipindi cha miezi ya Juni na Julai 2025 katika maeneo ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi na maeneo ya nchi kavu’ Alifafanuo Dkt. Chang’a.

 

Akitoa ushauri kwa sekta mbalimbali hapa nchini, Dkt. Chang’a alisema tahadhari za kiafya zinapaswa kuchukuliwa ili kulinda jamii dhidi ya magonjwa yanayoweza kusababishwa na baridi au vumbi, kwa wafugaji wanashauriwa kutumia maji na malisho kwa uangalifu, wakulima wakishauriwa kulima mbogamboga na mazao ya mizizi katika maeneo yenye unyevu au kwa maeneo yanayotarajiwa kupata vipindi vya mvua katika kipindi cha msimu wa Kipupwe. Kwa watumaiji wa bahari wanashauriwa kuendelea kufuatilia taarifa za hali ya hewa za kila siku kwa kuzingatia tahadhari na angalizo za hali mbaya ya hewa zitakazotolewa na Mamlaka, huku sekta ya madini, ujenzi na uchukuzi zikitarajiwa kunufaika zaidi na hali inayotarajiwa.

 

Kwa taarifa zaidi tembelea: https://www.meteo.go.tz/publications/single/575

 

Tuesday, April 22, 2025

WATAALAMU KUTOKA OFISI ZA UMOJA WA AFRIKA (AUC) WATEMBELEA TMA.

 




Dar es Salaam, Tarehe 17 Aprili 2025.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imepokea timu ya wataalamu  kutoka Ofisi za Umoja wa Afrika (AUC) wanaoratibu utekelezaji wa mradi wa kuboresha huduma za hali ya hewa wa “Intra-ACP Climate Services and related Applications Programme (ClimSA)”.

 Ziara hiyo ilifanyika tarehe 17 Aprili, 2025 ikioongozwa na mmoja wa Wasimamizi wa mradi wa ClimSA kutoka AUC Bw. Freddy Falanga (ambaye ni rai wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo), ambapo timu hiyo ya wataalamu walitembelea Ofisi Kuu ya Utabiri wa Hali ya Hewa, iliyopo Ubungo Plaza, Dar es salaam kwa lengo la kukagua utendaji kazi wa mitambo ya ufuatiliaji wa mifumo ya hali ya hewa na utabiri wa hali ya hewa, inayoitwa "PUMA STATION.", iliyotolewa kwa TMA kupitia mradi ClimSA.

Mradi wa ClimSA unatekelezwa katika nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AUC), ikiwemo Tanzania kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya (European Union). Mradi huu unalenga  kuimarisha zaidi uwezo wa nchi wanachama wa AU katika kufuatilia mifumo ya hali ya hewa kupitia teknolojia ya satelaiti ili kuboresha zaidi utabiri wa hali ya hewa na huduma za hali ya hewa kwa ujumla.

 Huduma hizi ni muhimu kwa  jamii na sekta za kiuchumi katika kupanga shughuli za maendeleo na kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi.

Tuesday, April 15, 2025

TMA YAPONGEZWA KWA UBORESHWAJI WA TAARIFA ZA HALI YA HEWA











Morogoro, Tarehe 15/04/2025

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imepongezwa kwa uboreshwaji wa utabiri wa hali ya hewa na taarifa za tahadhari za matukio ya hali mbaya ya hewa nchini. Hayo yamesemwa na Mhe. Dkt. Rozalia Rwegasira,  Kaimu Katibu Tawala Mkoa, sehemu ya uchumi na uzalishaji wa mkoa wa Morogoro wakati wa ufunguzi wa Semina ya Mradi wa Kuimarisha Uwezo wa Jamii Kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Hali ya Hewa na matukio ya Hali Mbaya ya Hewa, kwaajili ya Kupunguza Hasara na Uharibifu ,iliyofanyika mkoani Morogoro katika ukumbi wa NSSF, tarehe 15/4/2025.

“Utabiri wa hali ya hewa umeendelea kuboreshwa na tahadhari za mvua kubwa na matukio ya hali mbaya ya hewa zinatolewa kwa wakati na hivyo kuchangia kuokoa maisha ya watu na mali zao. Tunaishukuru na kuipongeza serikali kwa kupitia TMA kwa kazi hii njema”. Alisema Dkt. Rozalia.

Aidha, Dkt. Rozalia alitoa ahadi ya kushirikiana na TMA katika kufanikisha utekelezwaji wa mradi huu kwani utakuwa na faida kubwa na chanya kwa wananchi wa Tanzania.

“Katika kufanikisha utekelezaji wa Mradi huu, kwa niaba ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa tuanaahidi kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha kwamba wananchi wananufaika na taarifa  zitakazozalishwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kupitia Mradi huu, ili wadau na wananchi kwa ujumla kuweza kuchukua tahadhari kwa lengo la kupunguza athari zitokanazo na matukio ya hali mbaya ya hewa”.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA ambaye ni Mwakilishi wa Kudumu wa Shirika la Hali ya Duniani (WMO) na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC), Dkt. Ladislaus Chang'a aliishukuru Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuwekeza kwenye sekta ya hali ya hewa nchini.

“Nitumie fursa hii kutoa shukurani zangu za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuwekeza na kuisaidia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania katika kuimarisha huduma za hali ya hewa nchini kwa kuweka sera, mikakati na mazingira wezeshi yanachochea ubunifu na umahiri".

Dkt. Chang’a alisisitiza kwamba uwekezaji wa serikali kwenye miundombinu ya hali ya hewa nchini ndio chanzo kikuu cha uboreshwaji wa taarifa za hali ya hewa nchini na kuwasisitiza wananchi kuendelea kufuatilia  na kuzingatia taarifa za utabiri na tahadhari zinazotolewa na TMA, na pia kuzingatia sheria  ya Mamlaka ya Hali ya Hewa namba 2 ya mwaka 2019 na kanuni zake.

Mamlaka ya Hali ya Hewa inatoa shukrani za dhati kwa Tume ya sayansi na teknolojia (COSTECH) kwa kufadhili mradi huu muhimu ambao utaongeza ufanisi katika mchakato wa kukabiliana na mabadiliako ya hali ya hewa  na tabianchi nchini.

Tuesday, April 1, 2025

WATAALAMU WAJADILI MCHANGO WAO KATIKA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA HALI YA HEWA NA TABIANCHI












Wataalamu Wabobezi katika sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi wamekutana jijini Arusha katika kongamano la siku moja kwa lengo la kujadili mchango wao katika kukabiliana na mabadiliko hayo, tarehe 31 Machi 2025. 

 

Kongamano hilo limeandaliwa mahsusi kwa ajili ya kuongeza uelewa kuhusu shughuli za Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC); Ripoti zitakazoandaliwa katika  mzunguko wa saba wa IPCC (AR7) kuhusu tathmini ya mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi na fursa za kushiriki katika mchakato huo, ikijumuisha uandishi, uteuzi wa wataalamu na mapitio ya ripoti za IPCC. Vilevile kongamano hilo lilihamasisha wanasayansi hasa vijana, watendaji, wakufunzi na wanafunzi kufuatilia na kushiriki katika mchakato mzima wa shughuli za IPCC hasa katika mzunguko wake wa saba ulioanza mwaka 2023 na unatarajiwa kumalizika kati ya mwaka 2029 na 2030.

 

Kongamano limeratibiwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela, likijumuisha wataalamu wa sayansi ya mabadiliko ya hali ya hewa na tasnia zinazohusiana kutoka Tanzania na Afrika Mashariki. 

 

Mgeni rasmi katika ufunguzi wa kongamano  hilo alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TMA Mhe. Jaji Mshibe Ali Bakari ambaye kupitia hotuba yake alisisitiza ushiriki wa wataalamu wengi kutoka Afrika Mashariki katika mchakato wa IPCC. 

 

“Ni matumaini yangu kuwa kupitia makongamano kama haya ya uhamasishaji wa wanasayansi kujihusisha katika kufanya tafiti zinazokidhi matakwa ya IPCC, wataalam wengi zaidi kutoka Afrika Mashariki wataweza kutoa mchango wao kikamilifu katika utayarishaji wa ripoti za tathmini ya Saba ya mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi ya IPCC (IPCC AR7). Alisema Jaji. Mshibe 

 

Naye, Dkt. Ladislaus Chang’a, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na  Makamu Mwenyekiti wa IPCC  alielezea namna ambavyo ripoti za IPCC zimekuwa na mchango mkubwa katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi kimataifa na katika nchi moja moja. 

 

“Ripoti ya IPCC ya AR7 inayoandaliwa inatarajiwa kuwa ya kina na itakuwa na jukumu muhimu katika mustakabali wa hatua za kuchukua dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa natabianchi kwa kuzingatia taarifa za kisayansi zilizohakikiwa vyema ambapo zina mchango mkubwa katika kuongeza ustahimilivu dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi kikanda na Duniani kote”. Aliongeza Dkt. Changa.

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...