Dondoo
muhimu za mwezi Novemba, 2016
Taarifa hii inatoa uchambuzi wa mifumo ya
hali ya hewa kwa mwezi Oktoba, 2016 na mwelekeo wa viashiria vya mifumo ya hali
ya hewa pamoja na mvua katika kipindi cha mwezi Novemba, 2016.
- Mwelekeo wa
mvua za Vuli, 2016 kwa kipindi cha mwezi Novemba, 2016:
Hali ya
upungufu wa mvua inatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi katika kipindi cha
mwezi Novemba, 2016.
- Maeneo ya Nyanda
za juu Kaskazini mashariki pamoja
na maeneo ya mkoa wa Tabora mvua zinatarajiwa kuanza katika wiki ya
tatu ya mwezi Novemba,2016.
- Mvua za
wastani hadi chini ya wastani zinatarajiwa katika maeneo ya Ukanda wa Ziwa
Victoria, na mvua za chini ya
wastani katika maeneo mengine ya nchi.
 |
| Mkurugenzi Mkuu akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu mwelekeo wa mvua za vuli mwezi Novemba 2016 |