Saturday, May 16, 2026

KAMATI YA URATIBU YA MRADI WA SOFF YAKUTANA JIJINI DODOMA








Dodoma, 14 Mei 2026

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), kwa kushirikiana na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), walifanya kikao kazi cha tano cha Kamati ya Uratibu  wa Mradi wa SOFF (Systematic Observations Financing Facilit)  katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Kikao hicho kiliwakutanisha wataalamu muhimu ili kupitia maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa SOFF na kujadili vipaumbele vya kimkakati kwa mwaka 2026, vinavyolenga kuhakikisha ufanisi katika utekelezaji wa shughuli za mradi.


Majadiliano yalijikita katika utekelezaji wa Mpango Kazi wa Mwaka 2026,  ufuatiliaji na tathmini ya mradi, pamoja na shughuli za mawasiliano na uhamasishaji zilizopangwa kwa mwaka 2026. Kamati pia ilipitia maamuzi na maelekezo kutoka kikao cha Tatu cha Kamati Tendaji ya Mradi wa SOFF kilihofanyika Aprili 2026.


Wakizungumza katika ufunguzi, Wenyeviti wenza wa kamati hiyo, Dkt. Paschal Waniha kutoka TMA na Dkt.Abbas Kitogo kutoka UNDP, walisisitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiana kikamilifu ili kuhakikisha utekelezaji unafanyika kwa wakati katika shughuli zote zilizopangwa za mradi wa SOFF Tanzania.Aidha,

kikao kilihitimishwa kwa wajumbe kutoa dhamira ya pamoja ya kuimarisha uratibu, kuharakisha utekelezaji wa shughuli zilizopangwa, na kuongeza ufanisi wa jumla wa mradi wa SOFF nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...