WANAWAKE WA TMA WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI 2026, KWA KUFANYA SHUGHULI ZA KIJAMII.
Wanawake wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) wameadhimisha Siku ya Wanawake Duniani katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania kwa kufanya shughuli tofauti za kijamii zinazolenga kuimarisha mshikamano na kusaidia jamii.
Maadhimisho hayo yalifanyika kwa kuzingatia kaulimbiu ya mwaka huu isemayo: “Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana; Msingi Jumuishi kufikia Dira ya Maendeleo 2050.”
Katika Mkoa wa Dodoma, watumishi wanawake wa TMA walipata fursa ya kutembelea Kituo cha Watoto Yatima cha Safina kilichopo Ntyuka, ambapo walikutana na watoto wanaolelewa katika kituo hicho na kuwapa faraja pamoja na kuwasaidia kwa mahitaji mbalimbali.
Ziara hiyo ililenga kuonesha upendo, mshikamano na kuwapa matumaini watoto wasiokuwa na wazazi au wale wanaoishi katika mazingira magumu.





No comments:
Post a Comment