Mhe. Atashasta Nditiye akihutubia mkutano wa 18 wa
Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO)
|
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa 18 wa Shirika la
Hali ya Hewa Duniani (WMO)
|
Na: Christopher Philemon, Monica Mutoni. Geneva
11/06/2019.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawsailiano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye
ameeleza namna ambavyo Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) linavyochangia
katika uboreshaji wa huduma za hali ya hewa Tanzania. Mhe. Nditiye alizungumza hayo wakati
akihutubia mkutano wa 18 wa WMO, unaoendelea jijini Geneva, Uswisi.
‘WMO ina mchango mkubwa katika huduma za hali ya hewa nchini kama vile
miongozo maalum iliyowekwa kwa ajili ya uandaaji na utoaji wa tahadhari za hali
mbaya ya hewa kwa maeneo ya ziwa Viktoria ambapo TMA inatoa miongozo ya
tahadhari kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, utekelezaji wa Mfumo wa Kidunia
wa Huduma za Hali ya Hewa (Global Framework for Climate Services-GFCS) ambao
ndani yake Tanzania kupitia TMA inanufaika masuala mbalimbali kama vile mafunzo
ya muda mrefu na mfupi, upatikanaji wa baadhi ya vifaa vya hali ya hewa n.k’
alisema Mhe. Nditiye.
Aidha, katika hotuba yake, Mhe. Nditiye aliwasilisha salamu za Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na kuelezea namna
serikali inavyoweka jitihada kubwa kuhakikisha huduma za hali ya hewa nchini
zinakuwa za kisasa kwa kufanikisha ununuzi wa rada tatu za hali ya hewa pamoja
na kuifanya TMA iweze kukidhi zaidi matakwa ya watumiaji kwa kuibadilisha TMA
kutoka kuwa Wakala na kuwa Mamlaka kamili.
No comments:
Post a Comment