Matukio mbalimbali kwa picha wakati Sekta mbalimbali zikijengewa uwezo juu ya matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa katika halmashauri ya mji wa Kongwa |
Matukio mbalimbali kwa picha wakati waandishi wa habari wakijengewa uwezo juu ya matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa katika halmashauri ya mji wa Babati |
Chama cha Wataalam wa Hali ya Hewa Tanzania (TMS)
kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kupitia mradi wa “Weather and Climate
Information Services” (WISER), WISER, kiliweza kuwajengea uwezo wadau wa sekta
mbalimbali (Kilimo, ufugaji, nishati, maafa, maji pamoja na wanahabari) katika
halmashauri za miji ambazo ni Kongwa, Dodoma mjini, Hanang’ na Babati kwa kuendesha
mafunzo ya matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa kuanzia tarehe 27 Mei mpaka
31 Mei 2019.
Wageni rasmi katika mafunzo hayo, walikuwa ni wakurugenzi
wa halmashauri za miji ambao katika hotuba zao waliishukuru TMS kwa kuchagua kufanya
mafunzo hayo muhimu katika halmashauri zao. Aidha, wageni rasmi walihamasisha
kila mshiriki kupitia taaluma zao kuitumia vyema fursa hiyo adhimu waliyoipata
kwa kutambua namna ya kupata taarifa za hali ya hewa, kuzielewa kwa usahihi na
pia kuzifikisha kwa walengwa kwa wakati zitakazoimarisha mchango wa sekta ya
hali ya hewa katika kuongeza tija na ufanisi kwenye kilimo ambacho kina mchango
mkubwa wa kuzalisha malighafi kwa ajili ya Tanzania ya viwanda hivyo
utekelezaji wa programu hii utachangia katika kuunga mkono juhudi za Mh. Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dkt. John Pombe Magufuli za kulifikisha Taifa
katika uchumi wa kati na uchumi wa viwanda.
Kwa upande wa washiriki walikiri kupata uelewa kwa kiasi
kikubwa na kuahidi kuhakikisha taarifa
za hali ya hewa zinatumika kwa usahihi na kusambazwa kwa wakati ili kuwafikia
walengwa pamoja na kuweka nguvu kubwa
katika kushirikiana na TMA.
Malengo ya mafunzo hayo ni kuchochea matumizi ya taarifa
za hali ya hewa kwa sekta mahsusi zilizoainishwa katika mradi wa WISER na
kuwafikia wananchi wengi kupitia huduma ya taarifa za hali ya hewa inayotolewa
kwa njia ya simu za mikononi uitwao FarmSMS, ambapo zaidi ya wadau 600 walisajiliwa katika mfumo huo.
IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Tumia taarifa za hali ya hewa kwa maendeleo
ReplyDeleteendelevu
Delete