MWELEKEO WA MVUA ZA MACHI - MEI 2016
Kutokana
na mwelekeo wa mifumo ya hali ya hewa inayotarajiwa, mvua za Machi hadi Mei,
2016 zinatarajiwa kuwa kama ifuatavyo:-
(i)
Mvua za Masika
(kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua)
Msimu wa mvua za Masika
katika kipindi cha miezi ya Machi hadi
Mei, 2016 ni mahususi katika maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki (Mikoa
ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara), pwani ya kaskazini, (Mikoa ya Dar es
Salaam, Tanga, Pwani, Morogoro-kaskazini pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba), kanda ya Ziwa Victoria (Mikoa ya
Kagera, Mara, Mwanza, Geita, Simiyu na Shinyanga) na kaskazini mwa mkoa wa
Kigoma. Mvua hizo zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani kwa maeneo
mengi ya ukanda huo isipokuwa maeneo ya kusini mwa ukanda huo yanatarajiwa kuwa
na mvua za wastani hadi chini ya wastani.
Mwelekeo wa msimu wa mvua za Masika, 2016 ni kama
ifuatavyo:-
Kanda ya Ziwa Victoria:
(Mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, Geita, Simiyu na Shinyanga): Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza
ya mwezi
Machi, 2016 katika mikoa ya Kagera na Mara na kusambaa katika mikoa ya
Geita, Mwanza, Shinyanga na Simiyu katika wiki ya pili ya mwezi Machi 2016.
Mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo ya mikoa ya
Kagera, Mwanza, Mara na kaskazini mwa mkoa wa Geita. Kaskazini mwa mkoa wa Kigoma,
kusini mwa Geita na Simiyu, pamoja na mkoa wa Shinyanga mvua zinatarajiwa kuwa za
wastani hadi chini ya wastani.
Ukanda wa Pwani ya Kaskazini:
(Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Morogoro-kaskazini pamoja na Visiwa vya
Unguja na Pemba):
Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya pili hadi ya
tatu ya mwezi Machi, 2016 na
zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya
wastani katika maeneo ya kaskazini na mashariki mwa mkoa wa Tanga ; na Visiwa vya
Unguja na Pemba. Mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi chini ya wastani katika
mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro pamoja na maeneo ya kusini magharibi mwa mkoa wa Tanga.
Nyanda za juu Kaskazini
Mashariki: (Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara):
Mvua katika maeneo haya zinatarajiwa kuanza katika
wiki ya pili hadi tatu ya mwezi Machi,
2016. Mvua hizo zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi ya mikoa ya Arusha na
Kilimanjaro pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Manyara; na zinatarajiwa kuwa za
wastani hadi chini ya wastani katika maeneo mengi ya mkoa wa Manyara na kusini
mwa mkoa wa Arusha.
(ii) Mvua za
Msimu (Novemba – Aprili) kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua.
Mvua za msimu (Novemba hadi Aprili) ni mahususi kwa
maeneo ya Magharibi mwa nchi (Mikoa ya
Kigoma, Tabora, Katavi na Rukwa), kanda ya
kati (Mikoa ya Singida na Dodoma), nyanda za juu kusini-Magharibi (Mikoa
ya Mbeya, Iringa, Njombe na kusini mwa Morogoro), kusini mwa nchi na pwani ya
kusini (mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara). Mvua hizo zilianza mwezi Novemba 2015 na
zinatarajiwa kuendelea hadi mwezi Aprili,
2016. Katika maeneo hayo mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi chini ya
wastani katika maeneo mengi.
Kanda ya Magharibi (Mikoa ya
Kigoma, Tabora, Katavi na Rukwa):
Katika kipindi kilichobaki cha msimu, mvua
zinatarajiwa kuwa za wastani hadi chini ya wastani na zinatarajiwa kuisha mnamo
wiki ya nne ya mwezi Aprili, 2016.
Kanda ya kati (Mikoa ya
Singida na Dodoma):
Katika kipindi kilichobaki cha msimu, mvua
zinatarajiwa kuwa za wastani hadi chini ya wastani na zinatarajiwa kuisha mnamo
wiki ya kwanza ya mwezi Aprili, 2016.
Nyanda za juu Kusini
Magharibi: (Mikoa ya Mbeya, Songwe Iringa, Njombe na kusini mwa Morogoro):
Katika kipindi kilichobaki cha msimu, mvua
zinatarajiwa kuwa za wastani hadi chini ya wastani na zinatarajiwa kuisha mnamo
wiki ya tatu ya mwezi Aprili, 2016 katika maeneo ya mikoa ya Mbeya , Songwe na
Njombe na zinatarajiwa kuisha katika wiki ya kwanza ya mwezi Mei, 2016 katika
maeneo ya mkoa wa Iringa.
Maeneo ya kusini na pwani ya
kusini (Mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara)
Katika kipindi kilichobaki cha msimu, mvua
zinatarajiwa kuwa za wastani hadi chini ya wastani na zinatarajiwa kuisha mnamo
wiki ya pili ya mwezi Aprili, 2016.
No comments:
Post a Comment