Mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano
wa nane wa umoja wa taasis za hali ya hewa kusini mwa Afrika, Mkuu wa Wilaya ya
Monduli Mhe. Jowika Kasunga (wan ne kutoka kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa TMA
ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya MASA na mwenyeji wa mkutano huo Dkt. Agnes
Kijazi katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo.
Mamlaka
ya Hali ya Hewa kwa niaba ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
imekuwa mwenyeji wa mkutano wa kila mwaka wa umoja wa taasis za hali ya hewa
katika nchi za Kusini mwa Afrika (MASA). Mkutano huo unafanyika mkoani Arusha.
Akifungua mkutano huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha mgeni rasmi ambaye ni
mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Jowika W. Kasunga alizitaka taasis za hali ya
hewa kusini mwa Afrika ikiwemo TMA kushirikiana katika kutatua changamoto zinazoikabili
sekta ya hali ya hewa. ‘Wote tunakubaliana kwamba umoja ni nguvu, hivyo taasis
za hali ya hewa zinapaswa kudumisha umoja na ushirikiano ili kukabiliana na
changamoto zinazozikabili huduma za hali ya hewa kusini mwa Afrika’ alisema
Mhe. Kasunga.
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Hali ya Hewa ya Malawi na Mwenyekiti wa umoja huo alisema, lengo
kuu la mkutano huu ni kujaribu kutatua changamoto za taasis za hali ya hewa
kusini mwa Afrika.
Kwa
niaba ya TMA, Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi aliwakaribisha wageni
wote Arusha na kuwatakia majadiliano yenye mafanikio. Dkt Kijazi alisema ni
matarajio yake kwamba mkutano huo utatoa mapendekezo yatakayoweza kuboresha
huduma za hali ya hewa katika nchi za kusini mwa bara la Afrika.
IMETOLEWA
NA MONICA MUTONI - MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.
No comments:
Post a Comment