Wednesday, September 3, 2014

MKUU WA MKOA WA MOROGORO MHE.JOEL BENDERA AFUNGUA WARSHA YA WANAHABARI YA KUJADILI NAMNA YA UTOAJI WA UTABIRI WA MSIMU WA MVUA ZA OKTOBA HADI DESEMBA 2014

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Joel Bendera (aliyesimama) akizungumza na washiriki wa warsha (wanahabari) kuhusu umuhimu wa vyombo vya habari katika kuwafikisha wananchi taarifa za hali ya hewa akitoa mfano hai wa mafuriko yaliyoikumba Dumila mwanzoni mwa mwaka 2014.Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi na Dkt. Hamza Kabelwa (mwenye miwani) ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri-TMA
Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt.Agnes Kijazi akiongea na wanahabari katika warsha hiyo, Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa warsha hiyo.



Baadhi ya wanahabari wakichukua matukio ya ufunguzi wa warsha iliyoandaliwa na TMA kwaajili ya wanahabari.Warsha hiyo ilifunguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.


Baadhi ya wanawarsha (wanahabari) wakimsikiliza mgeni rasmi katika ufunguzi wa warsha iliyoandaliwa kwa ajili yao.

No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...